Meddie Kagere afunguka kuwakosa Singida United - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 30 October 2019

Meddie Kagere afunguka kuwakosa Singida United


Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa kushindwa kufunga ndani ya kikosi chake mchezo mmoja dhidi ya Singida United kwake si tatizo jambo la msingi ni pointi tatu muhimu.

Kwenye mchezo huo bao pekee la ushindi lilipachikwa kimiani na mzawa Miraji Athuman dakika ya 41 akimalizia pasi ya Mzamiru Yassin.

"Kufunga ama kutokufunga kwangu sio ishu ya msingi ama muhimu, tunachotazama tukiwa ni timu ni pointi tatu hizo ndio muhimu kwetu mambo mengine yatafuata," amesema.

Kagere ametupia jumla ya mabao saba ndani ya Simba ambayo aliyafunga kwenye mechi tano mfululizo alishindwa kufunga kwenye mechi dhidi ya Singida United iliyochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Simba imejikusanyia jumla ya pointi 18 ikiwa nafasi ya kwanza na haijapoteza mchezo hata mmoja ikiwa imeruhusu kufungwa mabao mawili pekee.

No comments:

Post a Comment