Waziri Kigwangalla amkingia kifua Mchekeshaji Idris Sultan - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 30 October 2019

Waziri Kigwangalla amkingia kifua Mchekeshaji Idris Sultan


Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka Mchekeshaji, Idris Sultan kufika katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu naye baada ya kufanyia ‘photoshop’ picha zake na kuweka kichwa cha Rais John Magufuli .

Hatimae Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala ameonesha kushangazwa na kitendo cha msanii huyo kuitwa polisi kwa kusema kuwa Rais Magufuli ni mtu wa watu na kwamba Idriss anafahamika kuwa sanaa yake ni ya uchekeshaji.

“Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo,” ameandika Kigwangala.

No comments:

Post a Comment