Achomwa kisu shingoni baada ya kummwagia mwenzie maji machafu siku ya 'birthday' - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Saturday, 16 November 2019

Achomwa kisu shingoni baada ya kummwagia mwenzie maji machafu siku ya 'birthday'


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma amethibitisha tukio la Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea, Grayson Maselin (23), kumjeruhiwa mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole (23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alidai tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya saa saba mchana katika chuo hicho.
Alidai kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.
Kamanda Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Kanisa Peramiho.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here