DC Komba akerwa Korosho nyingi kushindwa kufikishwa sokoni - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 25 November 2019

DC Komba akerwa Korosho nyingi kushindwa kufikishwa sokoni




Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba amewataka viongozi wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI watatue tatizo la uhaba wa vifungashio.
Komba alitoa agizo jana kwenye mnada wa korosho, uliofanyika katika viwanja vya ofisi kuu ya RUNALI mjini Nachingwea.
Alisema ni jambo lisilokubalika kuona korosho za wakulima zinashindwa kufikishwa sokoni kutokana na uhaba wa vifungashio.
Alisema hali hiyo itasababisha wakulima washindwe kuuza korosho zao kwa wakati, kufuatia hali hiyo amewataka viongozi wa chama hicho wahakikishe tatizo hilo linapata suluhisho, huku akimtaka mwenyekiti wa RUNALI, Hassan Mpako ambae alihaidi kwenda Dar-es-Salaam kufuata vifungashio kwa mzabuni ahakikishe anarudi na jibu la mwisho na iwe safari yake ya mwisho.
 ''Umesema mzabuni amesema kila kitu kipo sawa, sasa hakikisha unarudi na jibu la mwisho, vinginevyo hatutaelewana, nitafanya hivyo kwa ajili ya wakulima wetu,'' alisema Komba.
Alisema ni jambo la kusikitisha kusikia wanunuzi wanahitaji korosho nyingi lakini zilizopelekwa mnadani ni chache wakati nyingi zipo kwenye maghala ya vyama vya msingi vya ushirika ( AMCOS). Alisema, juzi chama hicho kilipokea gunia 30,000 na zimesambazwa katika baadhi ya AMCOS zilizopo katika wilaya za Ruangwa na Nachingwea. Huku akihaidi kwamba  wanatarajia kupokea gunia  nyingine 30,000 wakati wowote kuanzia hiyo jana.
Katika  mnada huo ambao ni wa nne kwa  msimu wa 2019/2020,  RUNALI kiliuza tani  2III.326.  Hata hivyo mahitaji ya kampuni 17 zilizo omba kununua yalikuwa tani 13967.130.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here