Iran kupunguza ahadi zake za mkataba wa nyuklia - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 5 November 2019

Iran kupunguza ahadi zake za mkataba wa nyuklia



Iran imesema itachukua hatua mpya katika kupunguza ahadi ilizotoa katika mkataba wa kihistoria wa nyuklia wa 2015 kuanzia kesho Jumatano kwa kuongeza gesi kwenye mitambo yake 1,044 ya urutubishaji Urani katika kiwanda chake cha Fordow.

Katika hotuba yake iliyorushwa leo kwenye televisheni, Rais Hassan Rouhani amesema hatua hiyo ni majibu ya moja kwa moja kwa rais wa Marekani Donald Trump kuiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia yaliotiwa saini mwaka 2015.

Katika makubaliano hayo Iran inaruhusiwa kuongeza viwango vya kurutubisha madini ya Urani japo bila kuongeza gesi kinyume na tangazo lililotolewa na Rouhani.

Jana Jumatatu Iran ilizindua mitambo aina ya 30 IR-6 ya kurutubisha madini ya Urani na kwa sasa taifa hilo lina mitambo 60 ya kisasa hali inayoonesha upeo na azma yake.

Mkuu wa shirika la nishati ya Atomiki nchini Iran Ali Akbar Salehi amesema Iran iliyokuwa inazalisha gramu 450 sawa na pauni moja ya madini ya Urani kwa siku, sasa itakuwa inazalisha kilo 5 ambayo ni sawa na pauni 11 kwa 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here