Miradi 32 ya matengenezo ya barabara kutekelezwa katika halmashauri za Lindi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 5 November 2019

Miradi 32 ya matengenezo ya barabara kutekelezwa katika halmashauri za Lindi



.

Miradi 32 ya matengenezo ya barabara inatarajiwa kutekelezwa katika halmashauri zote sita za mkoa wa Lindi katika mwaka wa fedha 2019\2020.

Hayo yameelezwa na meneja wa wakala barabara za vijijini na ijini wa mkoa wa Lindi, mhandisi Agatha Mtwangambate.  Alipozungumza na Muungwana Blog, jana mjini Lindi.

Mtwangambate alisema kwa mwaka wa fedha wa 2019\2020 miradi hiyo 32 inatarajiwa kutekelezwa katika halmashauri za Mtamama, manispaa ya Lindi, Liwale, Kilwa, Ruangwa na Nachingwea. Huku akiweka wazi kwamba utekelezaji wake upo katika hatua za kuweza kuanza. Kwani upo kwenye hatua ya kusaini mikataba.

Mhandisi Mtwangambate alizitaja kazi zilizopangwa na zinazotarajiwa kufanyika kuwa ni matengenezo ya muda maalumu kilometa 42.08 za sehemu korofi, kilometa 67.02 na matengenezo ya kawaida ni kilometa 386.29.

'' Lakini pia ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 75 kwa awamu ya kwanza, ujenzi wa boksi kalavati na vivuko vya miguu. Lengo kuu ni kuzifanya barabara za vijijini na mijini zipitike vipindi vyote vya mwaka,'' alisema  Mtwangambate.

Meneja huyo wa TARURA wa mkoa wa Lindi alisema katika mwaka wa fedha wa 2019/2020  wakala huo katika mkoa wa Lindi umeidhinishiwa shilingi 6,434,940,217.62 kutoka mfuko wa barabara kwa ajili ya matengenezo ya madaraja, barabara, matengenezo ya muda maalumu, sehemu korofi, kawaida, ujenzi wa mifereji na makalavati.

'' Lakini pia shilingi 1,800,000,000.00 toka mfuko wa maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa daraja linalounganisha baina ya wilaya za Liwale na Ruangwwa. Na ujenzi wa barabara kilometa mbili kwa kingo cha lami katika halmashauri za wilaya za Liwale na Ruangwa, kila upande zitakuwa na urefu wa kilometa moja,'' alisisitiza Mtwangambate.


Mbali na hayo, mhandisi Mtwangambate alisema TARURA mkoa wa Lindi  kwa mwaka wa fedha 2018\2019 uliingia mikataba mitatu kwa halmashauri za Ruangwa, Kiwa na Mtama kwa kazi ya matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 4.05 kwakutumia fedha za mfuko wa maendeleo( Devolpment fund).

Wakala wa barabara za vijijini na mijini katika mkoa wa Lindi unasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 4,130.29 ambazo zimehakikiwa na Kamati ya Taifa ya Upangaji wa Barabara katika madaraja(NRCC) na zimeingizwa kwenye  mfumo wa usimamizi na ufuatiliaji wa barabara( DROMAS). Kati ya hizo, kilometa 54.10 za lami, kilometa 665.17 za changarawe na kilometa 3,410 niza udongo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here