N
Kamati ya Sheria ,Utawala Bora na Idara Maalumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeshauri Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja kubuni na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza ukusanyaji wa mapato ndani ya Mkoa huo.
Ushauri huo ulitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zulfa Mmaka wakati wa majumuisho ya ya ziara yao katika ofisi za mkuu wa mkoa wa kusini Unguja zilizopo Tunguu.
Makamu Mwenyekiti huyo alisema kuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja inatakiwa kubuni vyanovingi vipya vya mapato ili kusaidia katika kukusanya mapato mengi zaidi nakuchochea ukuaji wa pato la taifa.
Alisema licha ya Mkoa huo kujitahidi katika kukusanya mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019 wanachotakiwa sasa hivi kubuni mbinu na vyanzo vingine vya mapato ambapo vitasaidia kukusanya mapato mengi zaidi na kuinua mkahuo kiuchumi.
“Natoa pongezi kwa mkoa huu kwa kufikia lengo la asilimia 100 katika kukusanya mapato lakini musiridhike kwa kiwango hicho mulichokusanya ni wajibu wenu sasa hivi kubuni vyanzo vingine vipa vya mapato ili kukusanya zaidi ya hichi” alisema Makamo mwenyekiti wa kamai hiyo.
Aliongeza kushauri ofisi hiyo kuhakikisha wanatafuta mbinu mbalimbali za kukabiliana na upotevu wa mapato unofanywa kamakasudi au kwa bahati mbaya.
“Serikali imekuwa ikibuni mirdi mbali mbali ya maendeleo nakutarajia kukusanya mapato kwakiasi kikubwa ila kumekuwepo na njia mbalimbali zinazopelekea kupotea kwamapato hivyo ofisi hii inatakiwa kubuni na kujua njia hizo kwa lengo la kunusuru mapato hayo” alisema Makamo Mwenyekiti.
Aidha Makamo mwenyekiti alishauri ofisi hiyo kutafuta namna ya kuondokana natatizo la dhalilishaji ambalo linaonekana kuwa likiathiri mkoa huo na taifa kwa ujumla.“Kiukweli tatizo la udhalilishaji bado ni kikwazo ndani ya mkoa nataifakwa ujumla hivyo kama kamati tunashauri ofisi kuanzia kwako mkuu wa mkoa kujenga mashrikiano kati yetu wakuu wa wilaya na wananchikwa ujumla ilikubaini wafanyaji wa hayo” alisema Makamo Mwenyeiti.
Hata hivyo kamati hiyo imempongeza mkuu wa mkoa wa kusini unguja kuwa imara katika kutekeleza mikakati mbali mbali ya maendeleo ndani ya mkoa huo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa alieleza kuwa Mkoa katika kutekeleza majukumu ya mamlaka ya Serikali za mitaa pamoja na ukusanyaji wa mapato kuanzia Aprili hadi Juni 2018/2019 kwa halmashauri ya wilaya ya kusini imekusanya jumla ya shilingi 47,883,440 kati shilingi 47,271,300 sawa na asilimia 101.
Aidha alieleza kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya kati jumla ya shilingi 195,680,300 wamekusanya kati ya shilingi 155,929,573 sawa na asilimia 125 ya iliyopangwa.
“Tumekusanya kisi hicho ambacho tumezidi malengo ambayo tumejiwekea katika kukusanya mapato kupitia halmashauri zetu” Alisema RC Ayoub.
Hata hivyo alisema ofisi yake itahakikisha kuwa wanafanya kila jitihada katika kupelekea mbele taifa kwa kuwatumikia wananchi katika sekta sote.
“Kwa upande wangu nitahakikisha kuwa sekta zote zinaenda sawa na kila mfanyakazi wa mkoa wa kusini atawajibika katika kuhamasisha kupiga vita vitendo vya udhalilishaji kwa watoto” alieleza mkuu huyo wa Mkoa.
Kwa upande wao wajumbe wakamati wakitoa michango yao walisema kuwa wamefurahishwa kwa utekelezaji wa mipango mbaimbali ya maendeleo yaliyofanywa ndani ya mkoa huo.
“Tumefurahishwa na kile ambacho tumekisikia kutoka kwenu ambacho mumekifanya katika kuwatatulia wananchi matatizo yao” walieleza wajumbe hao.
No comments:
Post a Comment