Waziri Hamad alisema maeneo yaliyoathirika zaidi na tatizo hilo ni Wilaya Micheweni kwa upnde wa Pemba na Mkoa wa Kaskazini Unguja ni maeneo ambayo yameonekana kutokea kwa vifo vingi vya kinamama na watoto.
Nae Mwakilishi Mkazi Bi Maha Damaj Shirika lake litalishughulikia suala na kufanya utafiti na kuhakikisha kwamba wanalipatia ufumbuzi na kujua sababu ya tatizo hilo katika maeneo hayo.
Aidha alisema kuwa yupo tayari kuitangaza Zanzibar na kuifanya kuwa ni kituo cha elimu ya malaria kutokana na mafanikio makubwa ya kutokomeza maradhi hayo kwa asilimia 0.2 jambo ambalo ni faraja kubwa duniani.
No comments:
Post a Comment