Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha SANGANIGWA CHILDREN HOME kilichopo Kigoma mjini Kenneth Hagize ametoa wito kwa jamii kuwa na desturi ya kutembelea mara kwa mara vituo hivyo kwani swala la kulea watoto yatima ni jukumu la kila mmoja.
Hagize ametoa wito huo ofisini kwake akizungumza na mwandishi wa na kusema kuwa wananchi wasiishie kutuma tu vitu bali wawe na desturi ya kutembelea kwani kuwatembelea watoto yatima huwatia moyo Zaidi watoto hao na kuona kuwa wapo karibu na jamii.
Aidha amesema kuwa kituo hicho kilianzishwa july 15/1995 ,ambapo kituo hicho kimesaidia watoto mbalimbali waliofiwa na wazazi wao ikiwemo wale ambao wazazi walikufa kwa majanga au maafa mbalimbali ndani na nje ya Kigoma.
Hata hivyo amesema kuwa zaidi ya watoto 115 wamesaidiwa na kituo hicho,ambapo watoto 70 wameshamaliza vyuo mbalimbali hapa nchini huku bahati mbaya 3 wakiwa wameshafariki.
Sanjari na hilo amesema ili mtoto aweze kupokelewa katika kituo hicho nisharti kuwepo barua kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa kisha afisa ustawi wa jamii kuthibitisha kusaidiwa kwa watoto hao ambapo ni kuanzia mtoto wa miaka 3 hadi 7 ndio wanaosaidiwa mpaka pale watakapo kuwa wanaweza 

Vilevile ameeleza kuwa katika kituo hicho wamekuwa wakijihusisha na kilimo cha umwagiliaji cha mbogamboga na matunda ili kuhakikisha wanapata fedha zitakazo wasaidia kununua mahitaji mengine ya vyakula kama mchele,maharage,mahindi ili kukidhi mahitaji mengine muhimu.
Mratibu wa kituo hicho amemalizia kwa kusema kuwa changamoto wanayokumbana nayo katika malezi ya watoto hao hasa katika makuzi yao ni kipindi cha umri wao wa kubarehe lakini amesema kuwa kama kituo wamepata kuwa na wataalamu wa kuwalea katika maadili na kuwafunza juu
ya mambo mbalimbali juu ya ukuaji waokujitegemea.

No comments:
Post a Comment