Yanga yasaka mshambuliaji mpya - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 4 November 2019

Yanga yasaka mshambuliaji mpya


Nyota anayekipiga timu ya Polisi Tanzania Ditram Nchimbi inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za kutua kwenye klabu ya Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo.

Yanga kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kusuka kikosi kipya kitakacholeta ushindani kwenye ligi baada ya kutolewa kimataifa na timu ya Pyramids jana kwa jumla ya mabao 5-1.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa tayari mazungumzo yameanza kufanyika ili kumpata nyota huyo asaidiane na David Molinga ambaye ameonekana kuingia kwenye mfumo wa Zahera.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Geofrey amesema kuwa hakuna tatizo kwa Yanga kuipata saini ya nyota huyo iwapo taratibu zitafuatwa.

"Kama wao wanamtaka Nchimbi hakuna shida maisha ya mchezaji ni kucheza sasa utaratibu upo wazi jukumu lao itakuwa ni kukaa mezani pia wanapaswa waongee na Azam FC ambao wao ndio mchezaji wao," amesema.

Nchimbi ametupia jumla ya mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara pia ni nyota aliyefanya vizuri kwenye michuano ya Chan nchini Sudan kwa kufunga bao la ushindi akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here