Medali mpya itakayo tumika kuwatuza maelfu ya wanariadha watakaoshiriki mbio za masafa marefu jijini Athens, Ugiriki yazinduliwa siku ya jana.
Jiji hilo la Athens linajiandaa kuwakaribisha wanariadha zaidi 60,000 kutoka nchi 120, mashindano hayo yatakafanyika kuanzia Novemba 10 mwaka huu.
Kila mwanariadha atakayemaliza mbio hizo ndani ya uwanja wa Panathenaic, ambao ulitumika kwa mbio za kwanza za olimpiki miaka ya 1896, atakabidhiwa medali hiyo ambayo inahashiria historia ya mbio hizo.
Rais wa shirikisho la riadha nchini humo, Kostas Panagopoulos amesema kuwa jumla ya medali 8 tofauti zitakabidhiwa mwanariadha mmoja kila mwaka hadi mwaka wa 2026 kusherehekea miaka 130 tangu kuzinduliwa kwa mbio hizo.
No comments:
Post a Comment