Rais Erdogan akutana na Trump - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 13 November 2019

Rais Erdogan akutana na Trump

Rais Donald Trump wa Marekani anamkaribisha rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan hii leo katika ikulu ya White House katika wakati ambapo nchi hizo zina mvutano kufuatia uvamizi wa kijeshi wa Uturuki nchini Syria lakini pia hatua ya Uturuki ya kununua mfumo wa Urusi wa kujilinda na makombora.
Wakuu hao wanakutana mwezi mmoja baada ya Uturuki kuanzisha mashambulizi ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Syria yaliyoruhusiwa na Trump na kuibua ukosoaji mkali wa bunge la Marekani lililotaka Uturuki kuwekewa vikwazo vikali.
Ikulu ya White House iliweka wazi kwamba lengo la Marekani ni kuzuia kurejea upya kwa waasi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS na si kukatisha mahusiano na wanamgambo wa Kikurdi wa nchini Syria.
Rais Erdogan alikiri ziara hiyo inafanyika wakati kukiwa na mahusiano mabaya kati ya washirika hao wa jumuiya ya kujihami ya Ulaya, NATO.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here