Hong Kong yazidi kukabiliwa na kitisho - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 13 November 2019

Hong Kong yazidi kukabiliwa na kitisho


Maafisa katika jiji la Hong Kong wamepandisha kiwango cha usalama kote kwenye jiji hilo kufuatia kuibuka upya kwa machafuko jana usiku.
Waandamanaji waliendeleza kampeni yao ya kuweka vizuizi barabarani na uporaji katika jaribio la kusitisha shughuli zote kwenye jiji hilo.
Wakati wa majira ya mchana ambayo huwa na shughuli nyingi zaidi ya waandamanaji 1,000 walizuia barabara kwenye mtaa wa kibiashara ulio katikati ya jiji hilo.
Afisa katika hospitali ya Hong Kong amesema mapema leo kwamba takriban watu 81 walijeruhiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
Mtu aliyepigwa risasi na polisi siku ya Jumatatu na mwingine aliyechomwa moto na waandamanaji bado wapo katika hali mbaya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here