Waziri wa Madini amsimamisha kazi Afisa Madini Arusha - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 13 November 2019

Waziri wa Madini amsimamisha kazi Afisa Madini Arusha




Waziri wa madini Dotto Biteko amemsimamisha kazi Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha Robert Erick  kutokana na kushindwa kusimamia soko la madini na kusababisha kupelekea Wafanyabiashara kuuza madini na kununua nje ya soko hilo kinyume cha sheria za madini.
Akizungumza mara baada ya kutembelea soko la madini na kujionea baadhi ya vyumba vilivyoko katika soko hilo vikiwa wazi bila wafanyabiashara hali iliyomsikitisha licha ya serikali kuanzisha soko hilo la madini bado wafanyabiashara hao hawalitumii soko hilo kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Aidha Biteko ameagiza kuwa hadi kufikia siku ya jumatatu wafanyabiashara wote wa madini wawe wamefika katika soko hilo ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku biashara za madini maeneo yasiyo rasmi ili serikali isipoteze mapato pamoja na kuzuia utoroshwaji wa madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini,  profesa saimon Msangila amesema kuwa kitendo amesema kuwa kitendo cha wafanyabiashara kutokutumia soko hilo kinazorotesha mchango wa sekta  hiyo katika maendeleo ya taifa na kuzua sintofahamu  ya biashara hiyo kufanyika kiholela bila kufuata sheria.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa madini Modest Emanuel  amesema kuwa wafanyabiashara hao wanakabiliwa na changamoto ya kutokua na leseni kutokana na kutokua na mitaji ya kutosha hivyo kushindwa kumiliki leseni hivyo ameimba serikali iweke utaratibu wa kulipia leseni kwa awamu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here