TCRA yahimiza wananchi kujitokeza kwenye Kampeni ya kusajili laini kwa alama za vidole - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Saturday, 16 November 2019

TCRA yahimiza wananchi kujitokeza kwenye Kampeni ya kusajili laini kwa alama za vidole




Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya Kati imewataka wakazi wa Dodoma kutumia fulsa ya kampeni ya umasishaji usajili kadi za simu unaoendelea jijini Dodoma, kusajili kadi zao za simu kabla ya tarehe ya mwisho ya kusajili Desemba 31.
Akizungumza na Muungwana Blog, Mkuu wa TCRA Kanda ya Kati, Antonio Manyanda, amewaomba wananchi kutumia fulsa hiyo ya Kampeni ya kuhamasisha watu kujiandikisha ambayo kwa Sasa wapo Dodoma.
"TCRA Kanda ya Kati  imeunda timu ambazo zinazunguka sehemu tofauti kuhamasisha jamii kusajili kadi zao za simu hivyo wananchi watumie fulsa hiyo kusajili kadi zao za simu kabla ya tarehe ya mwisho ya kukamilika kwa kampeni hiyo jijini hapa"
Ameongeza kuwa "Naomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwa ajili kukamilisha usajili wa kadi za simu kwa sababu ikifika Deseemba 31 hawatapa mawasilino," amesema Manyanda.
Amefafanua  kuwa TCRA inahitaji kuona kila mmoja amefanya usajili kwa njia ya alama ya vidole hasa ukizingatia teknolojia ya sasa inakuwa hivyo mahitaji mengi hususani ya kiofisi watu wanakamilisha kupitia simu.
Amesema kampeni kwa kanda ya kati wameanzia katika mkoa wa Singida ambapo wamefanikisha kwa asilimia kubwa kutokana na idadi kubwa ya watu wamejitokeza kushiriki katika kukamikisha usajili kupitia alama za vidole.
Amesema zoezi hilo limekamilika katika mikoa ya  Singida,Tabora na hivi Sasa wanaendelea katika  jijinDodoma na baadae kuelekeza Kigoma amesema jamii inapaswa kujua umuhimu wa kusajili kadi za simu kwa alama za vidole jambo litakalowasaidia kuwa huru katika matumizi ya simu zao.
Amesema kwa upande wa Dodoma wanatarajia kuhitimisha kampeni hiyo Wilayani Kondoa, kabla ya  hapo wanazunguka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, ambapo wataanza Novemba 27 kushawishi na kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kusajili kadi za simu kwa alama ya vidole.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wanasema zoezi ni zuri kinachokwamisha ni upatikanaji wa namba za vitambulisho vya NIDA, na kuomba kasi ya utolewaji wa vitambulisho iongezwe.
Ikumbukwe Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola, amehimiza NIDA kuharakisha zoezi hilo, na kuagiza namba hizo zipelekwe hadi Wilayani badala ya kusubiri wananchi wazifuate au kuzipata kwenye mitandao ya simu.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here