Hatupangi bei elekezi,Ukiona mahindi yamepanda bei kanunue mchele, huwezi basi usile - Waziri Hasunga - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Saturday, 16 November 2019

Hatupangi bei elekezi,Ukiona mahindi yamepanda bei kanunue mchele, huwezi basi usile - Waziri Hasunga



Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kuwa kuna malalamiko kuwa bei ya unga, mahindi yamepanda kwanini hawatengenezi bei elekezi kasema kama serikali haiwezi kupanga bei kwasababu wakati mkulima huyo analima alikuwa mwenyewe.
Amesema kuwa huyo mkulima alivyokuwa analima alikuwa mwenyewe hakuna aliyeenda, alipalilia mwenyewe na kuvuna mwenyewe wao kama serikali hawapangi
"Kuna malalamiko huko Watu wanasema mbona bei ya unga imepanda hamtengenezi bei elekezi, unatengenezaje bei elekezi wakati huyu mtu alipokuwa analima hakuna aliyekwenda alilima mwenyewe, kapalilia mwenyewe, kavuna mwenyewe unataka bei elekezi ya nini.?
"Hatupangi bei elekezi, ukiona mahindi yamepanda bei kanunue mchele,kanunue ndizi kama huwezi viazi, kama huwezi  na wewe kalime ukiona huwezi basi usile" amesema Waziri Hasunga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here