TIBA YA KISUKARI BAMIA - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 25 November 2019

TIBA YA KISUKARI BAMIA


TIBA ASILIA YA KISUKARI.Kisukari kimetokea kuwa miongoni mwa magonjwa yanayozidi kuwakumba watu wengi hasa wale walio na umri mkubwa kidogo na kwa kiasi kidogo vijana na watoto.Kuna aina mbili za kisukari : kisukari aina ya kwanza na kisukari aina ya pili .> Kisukari aina ya kwanza husababishwa na kuharibika kwa himoni inayoshughulika na ubadilishaji wa sukari mwilini.> Na kisukari aina ya pili husababishwa na hormone kushindwa kubadili sukari kwenda kwenye glaikojeni ambayo huweza kutunzwa kwa matumizi mengine ya mwili.Tiba za kitaalamu za kisukari zina gharama kubwa sana pia tiba hizi huwa sio za kudumu na hivyo mgonjwa hulazimika kuhudhuria kliniki ili kupata dawa zinazomwezesha kusisimua homoni zake, kimsingi sio dawa anazopewa bali ni vichocheo tu.
> Zifuatazo ni baadhi ya TIBA ZA ASILI za kisukari.1. Bamia. (Lady's finger au Okra)Bamia ni mimea ambayo hutumika kutengeneza mboga ya mlenda.
NAMNA YA KUANDAA> Chukua bamia (tunda) ambazo hazijakomaa ziambae kwa kuzikata sehemu ya mwisho na sehemu ya mwanzo ili ibaki sehemu ya katikati, kisha zipasue katikati ila usiziachanishe. Baada ya maandalizi hayo ziweke kwenye maji safi muda wa masaa 12 kisha asubuhi yake kunywa hayo maji kabla huajala chochote. Fanya hivyo kwa muda wa siku sita hadi nane.
NAMNA INAVYOFANYA KAZI.Nyuzi nyuzi laini (smooth fibers) ambazo zinapatikana katika bamia hufanya kazi ya kuzuia umeng'enywaji wa wanga na hivyo huzuia sukari kuongezeka kwenye chakula kupitia wanga zinazomeng'enywa.2. Mimea ya Hibiscus (Hibiscus plant)Hii ni mimea ambayo hutoa maua ya rangi tofauti tofauti kama meupe, mekundu, njano nk. Kama inavyoonekana katika picha:
NAMNA YA KUANDAA.> Chuma majani 20 ya mmea huo yasage yawe unga na uweke maji, kama una Brenda tengeneza juisi ya majani hayo. Iache muda wa masaa 12 Kisha kunywa asubuhi na jionivkwa mfululizo wa siku 8 bila kuacha. Ikitokea umesahau kunywa siku moja sitisha dozi hiyo na usubiri miezi miwili ipite kisha uanze upya.> Maua pia hutumika kama kiungo cha chai. Maua yake pia husaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama kisukari na magonjwa ya moyo. Saga maua yake na utumie kama kiungo kwenye chai japokuwa inakuwa na radha ya uchachu ila inasaidia.
NAMNA INAVYOFANYA KAZI> Husisimua na kuamsha insulini na kuifanya ifanye kazi kwa ufasaha zaidi.
Utafiti bado unaendelea na kadri siku zinavyoenda ndipo faida nyingi zaidi za mmea huu zinazidi kugundulika.
3. MATANGO.Matango ni mimea ambayo inatambaa ambayo ina matunda ya aina tofauti tofauti! Ipo mimea ambayo ina matunda marefu (Rod shaped) na yapo yenye umbo la duara yote hayo yana faida zinazofanana katika mwili wa binadamu.
NAMNA YA KUANDAATafuta matango ambayo yana rangi ya kijani!! (USIMENYE) 1.Osha na maji safi  2.katakata na maganda yake 3.kisha tengeneza juisi 4.kunywa kikombe kimoja cha ½ litre kunywa mara 2 kwa siku muda wa siku 30
NAMNA INAVYOFANYA KAZI.Nyuzi nyuzi laini (smooth fibers) ambazo zinapatikana katika bamia hufanya kazi ya kuzuia umeng'enywaji wa wanga na hivyo huzuia sukari kuongezeka kwenye chakula kupitia wanga Unaomeng'enywa.Pia kutokana na matango kutokuwa na sukari mtu mwenye kisukari anapotafuna anajaza tumbo na hivo huweza kuzuia hamu yake ya kula kitendo ambacho kitamsaidia kupunguza sukari katika mwili wake kwa kutokula mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here