Utoaji wa huduma za Vivuko nchini waboreshwa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 15 November 2019

Utoaji wa huduma za Vivuko nchini waboreshwa


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle amesema kuwa, Serikali imepiga hatua katika utoaji huduma za Vivuko kwa asilimia 131, huku huduma za karakana zikizidi kuimarika tangu Wakala huo uanzishwe mwaka 2005.
Mhandisi Maselle ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari, ambapo alikua akizungumzia utendaji kazi wa TEMESA katika kipindi cha miaka Minne ya Serikali ya awamu ya Tano.
 "Wakala umeendelea kuboresha na kusimamia uendeshaji wa vivuko vya Serikali nchini kwa kuongeza idadi ya vivuko kutoka 13 wakati Wakala unaanzishwa mwaka 2005 hadi kufikia 30 katika vituo 19 Tanzania Bara", amesema Mhandisi Maselle.
TEMESA pia imefanikiwa kununua vivuko vipya vitatu ambavyo ni MV Kazi kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni mkoani Dar es salaam kilichogharimu Shilingi Bilioni 7.3, MV Mwanza kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza kilichogharimu Shilingi Bilioni 8.9 na MV Tanga kinachotoa huduma kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga ambacho kimegharimu Shilingi Bilioni 4.02.
Ujenzi wa Vivuko vyote umegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 20.22 ambazo ni fedha za Serikali.
Mhandisi Maselle ameongeza kuwa pamoja na utoaji wa huduma za vivuko, Serikali imenunua boti ndogo Tano ambazo ni MV Tangazo inayotoa huduma ya dharura kati ya Kilambo na Namoto mkoani Mtwara, MV Kuchele inayotoa huduma ya dharura kati ya Msangamkuu na Msemo mkoani Mtwara, MV Mkongo inayotoa huduma kati ya Utete na Mkongo mkoani Pwani, MV Bweni inayotoa huduma za dharura kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga pamoja na MV Sar III ambapo ujenzi wa boti zote umegharimu Shilingi Milioni 415.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here