Wananchi Kahama kunufaika na kilimo cha Maembe - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 25 November 2019

Wananchi Kahama kunufaika na kilimo cha Maembe



Serikali ya halmashauri ya mji wa Kahama wilayani Kahama mkaoni Shinyanga imesema imepata wawekezaji watakaojenga viwanda vya kusindika matunda aina ya Maembe kwani yamekuwa yakipotea bila kuwa na faida kwa wananchi.
Akizungumza na mwandishi wa Muungwana blog afisa kilimo halmashauri ya mji wa Kahama Samson Sumuni amesema kila mwaka msimu wa Maembe unapofika matunda hayo yamekuwa yakipotea kwa kuharibika kwa kukosa soko ambalo ni la uhakika hivyo kwa sasa tayari halmashauri imetenga maeneo kwa ajili ya kujengwa viwanda vya kusindika matunda.
Sumuni amesema maeneo ambayo yametengwa ni mtaa wa Bukondamoyo uliopo Kata ya Mhungula, Nyashimbi pamoja na Mwendakulima huku halmashauri hiyo ikiendelea kuzungumza na wawekezaji wengine kwa ajili ya kuwekeza ili kuwa na vyanzo vingi vya mapato pamoja na kuinua uchumi kwa wananchi.
Amesema katika moja ya halmashauri hapa nchini zinazozalisha matunda aina ya Maembe kwa wingi halmashauri ya mji wa Kahama ni miongoni hivyo kujengwa kwa viwanda yatasaidia matunda hayo kupata soko sambamba na kuwa na upatikanaji wa bidhaa aina ya Juisi ya Maembe kuwepo.
Samson Sumuni amesema kuanzishwa kwa viwanda hivyo pia vitafungua fursa ya kilimo cha matunda kwa wakazi wa halmashauri kwani kwa sasa hawaoni faida ya kilimo hicho kwa kukosa soko hivyo wao kama wataalam wa masuala ya kilimo watahakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili matunda yapatikane kwa wingi ili wawekezaji wapate Maembe kwa wingi kwa muda wote.
Aidha amesema halmashauri ya mji wa Kahama imetenga eneo la ambalo halmashauri italima Kitalu chake cha matunda mbalimbali ambacho kitakuwa mfano kwa wakazi na wananchi kwa ujumla hivyo malengo ya halmashauri ni kuhakikisha matunda hayapotei bila faida.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here