CCM Nanyumbu wasikitishwa na malezi ya watoto - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 11 December 2019

CCM Nanyumbu wasikitishwa na malezi ya watoto



Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara kimetoa wito kwa wazazi na walezi wafuatilie mienendo ya watoto wanaowalea ili wawaepushe na mimba za utotoni.
Wito huo ulitolewa jana mjini Mangaka na katibu wa CCM wilaya ya Nanyumbu,  Didas Zembihile  wakati wa kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Zembihile alisema miongoni mwa sababu zinazosababisha mimba za utotoni ni baadhi ya walezi na wazazi kuwapa watoto wao uhuru usiona mipaka. Uhuru ambao unatumiwa vibaya kwani imeanza kuonekana sio jambo la geni wala aibu kuwaona watoto wanazurura mitaani usiku.
Katibu huyo alisema baadhi ya walezi na wazazi licha ya kushindwa kuwadhibiti watoto wao kuhusu vitendo vya uzururaji, lakini pia hawajui umuhimu wa elimu kwa watoto hao hali inayowafanya wawashawishi wafanye vibaya mitihani ili waolewe.
Alisema CCM kinatambua kwamba urithi bora kwa watoto ni elimu, kwa hiyo wazazi na walezi wenye tabia hiyo hawana budi kubadilika kwani hasara inayotokanana tabia hiyo siyo ya watoto wao tu, bali wazazi na walezi hao na taifa.
''Wazazi hatuna njia ya kukwepa lawama juu ya haya yanayotokea, watoto wanazurura mitaani usiku wa manane, wakibakwa na kupata mimba ni matokeo ya uzembe,'' alionya Zembihile..
Maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliandaliwa na shirika la msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto wa Lindi (LIWOPAC) kwa ufadhili wa mfuko wa huduma za kisheria (LSF).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here