Wafungwa 34 Masasi waachiwa kwa msamaha wa Rais Magufuli - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 11 December 2019

Wafungwa 34 Masasi waachiwa kwa msamaha wa Rais Magufuli




Wafungwa 34 wa Gereza la wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamekuwa ni miongoni mwa wafungwa zaidi ya 5000 waliopatiwa Msamaha wa raisi Dk.John Pombe Magufuli alioutoa disemba 9, 2019 katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru.
Aidha,wafungwa hao wamemshukuru raisi Dk.Magufuli kwa kuamua kutoa msamaha huo kwa wafungwa nchini na kwamba wao kamwe hawatofanya tena makosa pindi wakiwa uraiani na wao watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao katika jamii.
Wakizungumza hii leo (jana) wakiwa nje ya Gereza la wilaya ya Masasi,baadhi ya wafungwa hao walisema kwanza wanampongeza raisi Dk. Magufuli kwa kuamua kutoa msamaha huo na wao kuweza kwenda kukutana na ndugu,jamaa na rafiki zao bila ya kutarajia.
Halima Haidani alisema jambo muhimu ambalo wao kupitia msamaha huo wanalokwenda kulifanya katika jamii ni kuwa mabalozi kwa wengine kuhusu kuachana na vitendo vya uhalifu na kupelekea kufungwa gerezani.
"Kwanza tunampongeza raisi wetu Dk.John Magufuli kwa kutupatia msamaha huu ambao sisi wote hapa hatukutarajia kwamba leo tutakwenda kukutana na jamaa zetu huko nyumbani tunakupongeza raisi Dk.Magufuli, "alisema Haidani
Naye, Rujerere Juma alisema wakati wakiwa gerezeni alisikia kuwa raisi ametoa msamaha kwa wafungwa na yeye alimuomba mungu aweze kuwa ni mmoja kati yao wanaostahiki kupata msamaha na anashukuru amekuwa mmoja kati yao waliosamehewa.
Alisema alifungwa jela kwa kosa la wizi na kwamba sasa atarejea uraiani kwenda kuwa balozi mzuri kwa jamii.Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Masasi,Selemani Mzee alifika katika Gereza hilo kusimamia utekelezaji wa agizo la raisi Magufuli na kutoa rai kwa wafungwa hao 34 aliopata msamaha huo.
Alisema kwa vile wao 34 ndio waliopata masamaha huo wa raisi basi ni vema wanapokwenda katika jamii kwenda kuwa mabalozi wa amani na kuepuka vitendo vya uharifu.
Mzee alisema uraiani zipo shughuli nyingi za kiuchumi ambazo wao baada ya kupata msamaha huo wanaweza kwenda kuzifanya na kujipatia kipato badala ya kujiingiza katika vitendo ambavyo vitawafanya kufungwa kifungo jela.
"Nawasihi nendeni mkawe mabalozi wazuri katika jamii na msiwe watu wa kufanya vitendo vya uharifu alafu mkarudi humu ndani tena...zipo kazi huko nyingi za kuzifanya na mkapata fedha kihalali tendeni mkazifanye," alisema Mzee
Naye mkuu wa Gereza hilo la Masasi, SSP, Gibson Mwakibibi alisema Gereza hilo lina jumla ya wafungwa 160 lakini wafungwa ambao wamepata msamaha wa raisi ni wafungwa 34 akiwamo mwanamke mmoja kati ya hao.
Mwakibibi alisema wanaimani kwamba wafungwa hao watakwenda kuwa watu wema na wenye uzalendo kwa vile licha ya kufungwa lakini ndani Gereza hilo wamefundishwa kuwa wazalendo wazuri.
Alisema wapo baadhi ya wafungwa ambao wamepata msamaha huo lakini wanabadilika tena kuwa mahubusu kwa sababu wafungwa hao walikuwa na kesi zingine ambazo zinawakabili.
Mwakibibi aliwaomba wafungwa hao kwa vile wamepata msamaha huo wa raisi basi waende katika jamii kuwafunda wenzao ili kusiwe na watu wanaofungwa jela.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here