Faida zitokanazo na Mdalasini kiafya - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 December 2019

Faida zitokanazo na Mdalasini kiafya


Kutokana na thamani na umuhimu wa kiungo cha mdalasini inatosha kukifanya kiungo hiki kuwa moja ya mahitaji muhimu katika mlo wetu wa kila siku.
Mdalasini inasifika kwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya calcium, nyuzinyuzi  na madini chuma pia.
Moja ya sifa za kiungo hiki ni kuboresha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni pamoja na mzunguko wa damu mwilini.
Pia unapotumia kiungo hiki husaidia kuongeza homoni ya insulin kutengenezwa kadri ya mahitaji ya mwili na hivyo mhusika kuepuka madhara ya kisukari.
Jinsi ya Kutumia kiungo hiki kwa manufaa zaidi;Kila asubuhi chukua kijiko kimoja cha unga wa mdalasini, kisha changanya na kijiko kidogo kimoja cha asali na kuongeza robo kikombe ya juisi ya embe kisha changanya halafu tumia mchanganyiko huo.

Tumia mchanganyiko huo kila siku asubuhi kwa muda wa mwezi mmoja na utaona mabadiliko ya matatizo mbalimbali yakiafya yakiwemo hayo yaliyotajwa hapo juu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here