Mifuko mbadala isiyokidhi viwango marufuku nchini - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 6 December 2019

Mifuko mbadala isiyokidhi viwango marufuku nchini




Serikali imesema kamwe haitaruhusu uzalishaji, uingizaji na matumizi ya mifukombadala aina ya Non-Woven isiyokidhi viwango vya 70 Gram Per Square Metre (GSM)kutumika nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mussa Sima katikaMkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezajiuliolenga  kusikiliza na kutatua changamoto zao, Mkutano uliofanyika katika ukumbi waChuo cha Uuguzi Kibaha mkoa wa Pwani.
Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiloamesema kuwa kumekuwa na uchelewashaji wa utoaji wa vibali vya kuingiza mifukombadala nchini kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira haliambayo inaleta vikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji.
Akitoa ufafanuzi wa ucheleweshaji wa vibali hivyo Mhe. Sima amesema kuwa Serikaliimepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini tangu Juni Mosi 2019 na kutoafursa kwa wakezaji kuagiza na kuzalisha mifuko mbadala ili kukidhi soko la ndani.
Hata hivyo changamoto imejitokeza kwa wafanyabiashara wasio waaminifu kutakakuingiza mifuko isiyokidhi viwango aina ya Non-Woven.
“Kumeanza kujitokeza uvunjifu wa sheria katika uzalishaji na uingizaji wa mifuko mbadala aina ya non-woven. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeweka vigezo vya mifuko mbadala aina ya non-woven inayoweza kutumika nchini ikiwa ni pamoja na Uzito usiopungua GSM 70 (Gram perSquare Metre), iweze kurejelezwa, Ioneshe uwezo wa kubeba, anuani ya mzalishaji naiwe imethibishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)” Sima alifafanua.
Amesisitiza busara itumike katika kumaliza mgogoro uliopo baina ya mfanyabiasharaaliyeagiza bidhaa hiyo huo bila kuathiri upande wowote kwa kutoa mapendekezo kwa√mfanyabiashara mwenye mzigo husika kuurejereza ama kuusafirisha nje ya chini yauangalizi maalumu na kuagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) na Shirika la Viwango nchini (TBS) kumaliza suala hilo mapemaiwezekanavyo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Sima amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Raisimefanya mapitio ya Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009 na kutunga Kanuni mpyaya mwaka 2019 ambazo zimezingatia Mkataba wa Basel yaani Basel Convention fortransboundary Movement of Hazadous Waste ambao Tanzania imeridhia baada yaawali biashara hiyo hairatibiwi ipasavyo.
“Kwa mujibu wa Mkataba huu, mfanyabiashara anapotaka kuingiza Hazadous Wasterikiwemo chuma chakavu pamoja na masharti mengine ni lazima nchi ambapo chumachakavu kinatoka kupata kibali cha Serikali ya nchi husika ili kuthibitisha kuwa nchi hiyoimeruhusu usafirishaji huo” Sima alisisitiza.
Amefafanua kuwa malighafi inayotumika na Viwanda vya ndani imekuwa ikipelekwa nje,hivyo Serikali imeweka masharti magumu kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani nakuruhusu kusafirishwa kwa malighafi ambayo haitumiki hapa nchini.
Naibu Waziri Sima amewahimiza wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Pwani nakutumia nishati ya gesi kwa wingi.
“Ni viwanda 48 tu nchi nzima ndio vinatumia nishati ya gesi, wawekezaji wekeni nia ya matumizi ya Gesi ili TPDC waweke miundombinu stahiki, nawasihi ndugu zangu tulinde mazingira yetu” amesema.
Siku ya pili ya mkutano wa Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na washiriki kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here