Polisi na waandamanaji wakabiliana Hong Kong siku ya Krismasi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 26 December 2019

Polisi na waandamanaji wakabiliana Hong Kong siku ya Krismasi



Sherehe za Krismasi katika mji wa Hong Kong, zimekumbwa na vurugu kufuatia makabiliano yaliyotokea, kati ya polisi na waandamanaji wanaotaka uhuru na demokrasia zaidi, huku kiongozi wa mji huo anayeunga mkono China akisema sherehe hizo zinavurugwa na waandamanaji.
Polisi walitumia gesi za kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliokusanyika katika maeneo ya maduka na katika mitaa kadhaa mjini humo ili kuwatawanya.
Vijana kadhaa waandamanaji, walikamatwa na maafisa wa polisi waliovalia kiraia ambao walikuwa kati ya waandamanaji. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti katika vituo kadhaa vya televisheni mjini humo.
 Hata hivyo vurugu za leo hazikudumu kwa muda mrefu kama vurugu za Mkesha wa Krismasi ambapo makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yalidumu kwa masaa kadhaa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here