Waliosoma na RC Gaguti IFM wafanya kitu cha tofauti kwa wazee na yatima Kagera - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 26 December 2019

Waliosoma na RC Gaguti IFM wafanya kitu cha tofauti kwa wazee na yatima Kagera





Umoja wa wanagroup la whatsapp waliosoma katika chuo cha fedha na mipango IFM wametoa msaada wa chakula na vinywaji wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki moja katika kituo cha kulelea watoto yatima na kituo cha kulelea wazee kihilima vilivyopo Bukoba mkoani Kagera ikiwa ni kumuunga mkono mwanafunzi mwenzao ambaye ni mkuu wa mkoa Kagera Bri. Jen. Marco E Gaguti katika kuhakikisha anatekeleza vizuri mipango yake.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya wanakikundi hao waishio Dar es salaamu bw. Edwini Mgoa amesema kuwa ni utamaduni wao kama kikundi kila mwisho wa mwaka kutoa misaada hiyo kwa makundi mbalimbali yasiyojiweza ili kuhakikisha na wao wanasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka vizuri na kuwatia moyo katika maisha yao.
"Kuna umuhimu wa kuwa tunatoa sadaka kwa ajiri ya wahitaji make wengi tumekuwa tukikutana kwenye vikundi hivi kwa ajiri ya kunywa na kufurai lakini tunasahau kuwa kunawahitaji kwahiyo tukumbuke kuwa kupitia mahusiano yetu haya kuna watu wanaweza kunufaika na kufurai kwahiyo tusiwasahau wazee na watu wengine wenye uhitaji" Amesema Edwini.
Akipokea misaada hiyo na kwa niaba ya serikali ya mkoa Kagera afisa ustawi wa jamii mkoa wa Kagera bi, ,Rebeca Gwambasa amewashukuru wanagroup hao na kuwaomba watu wengine wenye magroup kama hayo kuiga mfano huo kwani wapo watu wengi wenye uhitaji na hawana uwezo.
Kwa upande wake mama mlezi wa kituo cha kulelea wazee cha Kihilima kilichopo halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera amewashukuru wanaumoja wa group la whatsapp waliosoma na mkuu wa mkoa Kagera Bri. Jen. Marco E Gaguti kwa kujitoa na kuwasaidia wazee hao make wameonesha upendo wa aina yake katika kusherehekea siku ya christmas na mwaka mpya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here