Waziri wa Nigeria apendekeza adhabu kali zaidi kwa wabakaji - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 6 December 2019

Waziri wa Nigeria apendekeza adhabu kali zaidi kwa wabakaji



Waziri wa Wanawake nchini Nigeria Pauline Tallen ametoa wito wa adhabu kali izidi kutolewa kwa watu wanaofanya vitendo vya ubakaji, ikiwa na lengo la kuondoa tatizo hilo na aina zote za uhalifu dhidi ya wanawake na watoto.
Tallen amesema hayo wiki moja baada ya Mamlaka ya Taifa ya Kudhibiti Biashara Haramu ya Kusafirisha Binadamu, kuongeza kampeni dhidi ya uhalifu wa kijinsia kwa kuzindua kitabu cha kuandikisha wanaofanya vitendo hivyo.
Amesema karibu wasichana milioni 2 nchini Nigeria wanafanyiwa uhalifu wa kijinsia kwa mwaka, na kwamba ni asilimia 28 ya vitendo hivyo ndio imeripotiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here