Liberia yarejesha shehena za takataka hatari za plastiki zilikotoka nchini Ugiriki - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

KABATA2

Saturday, 11 January 2020

Liberia yarejesha shehena za takataka hatari za plastiki zilikotoka nchini Ugiriki



_110472904_c37cc573-f767-40c8-b08c-43fbac4c722dMamlaka ya Liberia imesema kwamba inarejesha shehena nne nchini Ugiriki zilizojaa tani za mifuko ya plastiki ambayo ni hatari kwa mazingira.
Mifuko hiyo ilikuwa imeingizwa nchini humo kimagendo "kwa kisingizio kwamba inaweza kuchakatwa upya".
Maafisa wa kupambana na bidhaa zinazoingizwa kimagendo nchini humo, waliibua malalamishi yao katika bandari ya Monrovia pale mzigo ulipowasili ukiwa unanuka "uvundo", na kutoa harafu mbaya, amesema mkuu wa Shirika la Kulinda Mazingira, Nathaniel Blama,
Aidha uchunguzi umeanzishwa mara moja kuhusu namna mzigo huo ulivyoagizwa.
Baada ya kontena hizo kukaguliwa, shirika hilo limesema kuwa aina ya mifuko ya plastiki iliyoletwa, imepigwa marufuku kuchakatwa na kutumiwa tena nchini Ugiriki.
Inaaminika kwamba mifuko hiyo ambayo haiwezi kutumika ilikotoka, iliuziwa dalali mmoja wa eneo ambaye aliinunua na kupanda usafiri wake.
Maili 350 ya Pwani ya Liberia ina lindwa na maafisa wa kushika doria na mara nyingi meli za uvuvi za kimataifa huingia eneo hilo kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad