Daktari aeleza ugumu wa kubaini TB kwa watoto - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 26 April 2021

Daktari aeleza ugumu wa kubaini TB kwa watoto

 

Hayo yameelezwa leo Aprili 26 na mratibu wa kifua kikuu  na ukoma mkoani Pwani Dk Aden Mpangile wakati akizungumza na mwananchi kuhusu namna ya ugunduzi wa ugonjwa huo kwa watoto wadogo na waliopo shule za msingi.Ameyataja magonjwa yanayofanana na TB kwa dalili kuwa pamoja na utapiamlo, dalili za mtoto aliyepata maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU )  kichomi au Nimonia kwa hiyo  mtu mwingine anaweza kufikiri mtoto mwenye  TB  anasumbuliwa na dalili za magonjwa mengine.Amesema mpaka sasa Serikali imeweza kugundua wagonjwa kwa asilimia 59 tu hivyo kuna deni la wagonjwa asilimia 41 ambao inabidi watafutwe.Dk Mpangile amesema miongoni mwa makundi yanayoathirika na TB ni watoto wa umri wa miaka 0 -14,  kundi ambalo wamo pia wanaokua kwenye shule za msingi.Watoto hao kulingana na malengo ya  Umoja wa Mataifa, kila watu 100 pawepo watoto 15 ambao waliogundulika na kwa nini iwe hivyo, kwa sababu watoto wanaishi na wazazi wenye ugonjwa, hivyo uwezekano wa wao kuambukizwa ni mkubwa," amesema Dk MpangileDk Mpangile amebainisha kuwa kuna hatua mbalimbali zimechukuliwa kuweza kugundua watoto wenye TB , moja wapo ni kuwachunguza watoto wote wanaokohoa na wanaooneka wana lishe duni ambapo katika kufanya uchunguzi wanaangalia mambo mengi ikiwemo historia ya mtoto, kupata homa za mara kwa mara,kikohozi kisichoisha, kutoongezeka au kupungua uzito na kumchunguza  uti wa mgongo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here