Profesa Kabudi atoboa siri ya kudumu kwa Muungano - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 26 April 2021

Profesa Kabudi atoboa siri ya kudumu kwa Muungano

 

waasisi wa Taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Karume.


Ameyasema hayo leo Aprili 26, katika kongamano la miaka 57 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar jijini Dodoma lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango.


Aidha waziri huyo amesema kuwa miungano mingi ya hiyari imekufa isipokuwa Tanganyika na Zanzibar hii ni kutokana na nchi hizo mbili kuwa huru na kulinda nafasi na maslahi maalum ya muungano na kuwepo kwa ushirikiano na utaratibu mzuri miongoni mwa mataifa hayo.


“Hayati MwalimuJulius Nyerere aliazimia kuunda taifa moja lenye mshikamano na kuwaunganisha Wazanzibar pamoja na Watanganyika,” amesema Profesa Kabudi huku akirejea kitabu kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere cha Freedom and Unity cha mwaka 1963.


Hata hivyo, Kabudi amesisitiza kuwa nchi inapaswa kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio kuikatisha kama wengi walivyozoea kutamka Tanzania.


Waziri huyo pia amesema kuwa muungano huu ni wa mshikamano, ushirikiano na pia kulikuwa na nia na sababu ya mataifa haya kuungana na ndio maana tunatawaliwa na katiba na sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here