Dkt. Magembe: Timu za uendeshaji wa huduma za afya timizeni wajibu wenu - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 26 April 2021

Dkt. Magembe: Timu za uendeshaji wa huduma za afya timizeni wajibu wenu

 

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha miaka 57 ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,001 waliokuwa wakaitumikia adhabu ya vifungo mbalimbali.Kati ya wafungwa hao,  1,516 wameachiwa huru baada ya kupunguziwa robo ya adhabu zao badala ya punguzo la kawaida la theluthi moja linalotolewa chini ya kifungu cha sheria ya Magereza sura ya 58.

Wafungwa wengine 3,485 wamepunguziwa robo ya adhabu zao badala ya punguzo la kawaida la theluthi moja linalotolewa chini yakifungu cha 49(1) cha Sheria ya Magereza sura ya 58.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa wafungwa 3,485 waliopunguziwa adhabu zao wataendelea kutumikia sehemu ya kifungo iliyobaki.

Kupitia taarifa hiyo, Rais Samia amewataka wafungwa wote walioachiwa huru kutumia vyema mafunzo walyopata wakiwa gerezani na waungane na wanachi wenzao katika ujenzi wa taifa huku wakiheshimu na kuzingatia sheria za Taifa.

“Pia niwaombe Watanzania ni vyema mkatumia siku ya maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano kutafakari juhudi mbalimbali zilizofanywa katika ujenzi wa taifa na wajibu wa kila mmoja katika kuendelea kujenga taifa imara,” amesema Samia


Pia ameahidi kuendelea kuuenzi, kuulinda na kuendeleza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa manufaa ya Watanzania wa pande zote mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here