EU yalenga kuiwekea Belarus vikwazo kufuatia kisa cha 'utekaji' ndege - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 28 May 2021

EU yalenga kuiwekea Belarus vikwazo kufuatia kisa cha 'utekaji' ndege

 


Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, amesema mapendekezo yako mezani kuzilenga sekta muhimu za uchumi wa Belarus. Alisema hayo jana baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje mjini Lisbon. 

Hii ni kufuatia kisa cha ndege ya abiria kulazimishwa kutua nchini Belarus. Hatua iliyosababisha baadhi ya mashirika ya ndege ya Ulaya kuamua kuepuka anga ya Belarus. 

Mzozo huo umetanuka baada ya Urusi kudaiwa kuzuia baadhi ya ndege za Umoja wa Ulaya kutumia anga yake. Umoja huo unaandaa jibu lake baada ya viongozi wa nchi 27 wanachama wake, kuridhia kwamba utawala wa rais wa Belarus Alexander Lukashenko uwekewe vikwazo.

Awali Borrell alidokeza uwezekano wa kulenga sekta ya mbolea au kukataa gesi ya nchi hiyo inayouziwa Umoja wa Ulaya. 

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Heiko Maas pia alidokeza uwezekano wa kulenga sekta ya mbolea. Mapendekezo hayo ya vikwazo ni kufuatia kisa kilichotajwa kuwa 'utekaji' wa ndege na utawala huo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here