Nchini Vietnam kumegunduliwa mripuko mpya wa virusi vya corona, ambao unasambaa kwa kasi hewani. Aina hiyo mpya ni mchanganyiko wa virusi vya kwanza pamoja navirusi vya india na Uingereza.
Waziri wa Afya wa Vietnam, Nguyen Thanh Long amenukuliwa na vyombo vya habari akisema pamoja na sifa ya kusambaa kwa kasi, virusi hivyo vina uwezo wa kulizonga koo kwa haraka na vilevile kuenea kwa kiwango kikubwa katika mazingira.
Waziri huyo hakutaja idadi ya maambukizi mapya yaliyothibitishwa kutokana na virusi hivyo, lakini aliongeza kusema kuwa hivi karibuni Vietnam itautangazia ulimwengu juu ya aina hiyo mpya virusi vya corona.
Vietnam yenye jumla ya watu milioni 97 kwa sasa inakabiliana na janga la virusi vya corona ambapo mpaka sasa watu wapatao 6,700 wameambukizwa na wengine 47 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.
No comments:
Post a Comment