Wayahudi wa Orthodox waipinga Israel - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Saturday, 29 May 2021

Wayahudi wa Orthodox waipinga Israel

 


Wayahudi wa Orthodox waliandamana kupinga utawala na sera za Israel katika Jiji la New York nchini Marekani (USA).


Mamia ya Wayahudi wa Orthodox walikusanyika kufanya maandamano katika jiji la New York kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina na kuwaunga mkono Wapalestina.


Waandamanaji hao walibeba mabango yaliyoandikwa, "Kupinga Uzayuni sio kupinga Uyahudi" na kuandamana kwenye Daraja la Brooklyn huku wakitoa kaulimbiu zinazosema, "Taifa la Israel haliwakilishi Wayahudi."


Rabi Hershel Klar, mmoja wa viongozi wa jamii ya Wayahudi wa Orthodox, alisema katika taarifa kwamba mvutano wa hivi karibuni kati ya Israel na Palestina pia umeonekana katika jamii zao.


Katika taarifa yake alisema,"Wayahudi wote wanadhaniwa kuunga mkono taifa la Israel, lakini sivyo ilivyo. Jamii yetu inapingana na Israel na inalaani vita vyake."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here