IGP Sirro awataka Askari Polisi kutenda haki - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 28 May 2021

IGP Sirro awataka Askari Polisi kutenda haki

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka askari kuhakikisha wanaendelea kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kushirikiana nao katika kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.

IGP Sirro amesema hayo Dar es salaam, wakati akizungumza na baadhi ya wananchi  wa eneo la Kawe wilaya ya Kinondoni ambapo aliwataka wananchi kuacha kutoa rushwa kwani kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali hasa watendaji wa kata na wenyeviti wa serikali za mitaa kuwashirikisha wananchi katika vikundi ya ulinzi shirikishi ili maeneo yao yaendelee kuwa salama.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here