China imesema inaunga mkono uchunguzi kamili wa aina zote za virusi vya corona vilivyogunduliwa ulimwenguni kote.
Kupitia mwakilishi wake katika ubalozi wa Washington, China imesema pia kuwa inaunga mkono uchunguzi kabambe dhidi ya baadhi ya vituo vya siri vya kibaolojia na maabara ulimwenguni kote.
Kauli hizo zinajiri baada ya Marekani kuitolea mwito Shirika la Afya Duniani WHO, kufanya uchunguzi wa pili kubaini vyanzo vya virusi vya corona na wataalamu huru wapewe idhini kamili kupata data za awali na sampuli nchini China.
Mnamo Jumatano, rais wa Marekani Joe Biden aliwaagiza maafisa wake kutafuta majibu kuhusu chimbuko la virusi hivyo akisema mamlaka za intelijensia za Marekani zinafuatilia natharia kuhusu virusi hivyo ikiwemo uwezekano kwamba vilisababishwa kutokana na ajali kwenye maabara nchini China, akidai uchunguzi wa awali haukuwa kamilifu.
Timu ya wataalamu walioongozwa wa WHO kufanya uchunguzi kwa miezi minne kati ya Januari na Februari pamoja na watafiti wa China, walisema kwenye ripoti yao kwamba huenda virusi hivyo vilitoka kwa popo hadi kwa mnyama na hatimaye kwa wanadamu.
Pia walisema hakukuwepo ishara bayana kuwa virusi hivyo vilitoka katika maabara.
No comments:
Post a Comment