Kocha mkongwe anayeheshimika Uingereza Roy Hodgson ataondoka katika timu ya Crystal Palace mwishoni mwa msimu huu.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya klabu hiyo kutokuonesha dalili ya kumuongezea mkataba mpya wakati mkataba uliopo sasa ukielekea kumalizika,Kocha huyu mzoefu ambaye amepata kuifundisha pia timu ya Taifa ya Uingereza amedumu kwenye klabu hii kwa miaka 4.
''Kwa sasa basi tena mambo ya soka nakwenda kuwa karibu zaidi na mke na familia yangu, shughuli za soka ziliniweka mbali na familia kwa muda mrefu,naona muda umefika kujikita zaidi kwenye familia,'' alisema Hodgson.
Naye Mwenyekiti wa timu hiyo Steve Parish amethibitisha kuachana na Hodgson na msaidizi wake Ray Lewington lakini amewashukuru fanya kazi pamoja kwa miaka yote minne akielezea furaha yake kufanya kazi.
Hodgson alianza kazi ya ukocha mwaka 1976 katika timu ya Halmstad ya Sweden kwa miaka 4 na amemalizia kwenye klabu ya Crystal Palace 2021 akiwa amedumu kwa miaka 45, mafanikio yake makubwa ilikuwa ni kuifanikisha Inter Milan kucheza fainali ya'European Cup' 1996-1997 lakini wakapoteza kwa Schalke 04.
Hodgson ameiacha timu hiyo kwenye nafasi ya 13 ikiwa na alama 44 ikiwa imebakiza mechi 2 huku timu zilizoshuka tayari zikiwa zimejulikana ambazo ni Sheffi
eld United, West Bromwich Albion na Fulham.

No comments:
Post a Comment