BAADA ya ratiba ya Ngao ya Jamii kuwa wazi na ikitarajiwa kuchezwa Septemba 25 kati ya Simba v Yanga, leo Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) imeweka hadharani ratiba ya ligi.
Ratiba inaonyesha kwamba Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 27 ambapo ni Mtibwa Sugar v Mbeya Kwanza, Uwanja wa Jamhuri, Moro.
Namungo v Geita utapigwa Uwanja wa Ilulu.
Coastal Union v Azam FC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Hizi hapa zitapigwa Septemba 28:-
Dodoma Jiji v Ruvu Shooting, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mbeya City v Mbeya City ngoma itapigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Biashara United v Simba SC, Uwanja wa Karume, Mara.
Polisi Tanzania v KMC ngoma itapigwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.
Kagera Sugar v Yanga ngoma itapigwa Uwanja wa Kaitaba.
Yanga na Simba hizi mechi zao za ufunguzi zote watakuwa ugenini huku mchezo wao wa Kariakoo Dabi kwenye ligi ukitarajiwa kuchezwa tarehe 11/12/2021.

No comments:
Post a Comment