SIMBA:KILA KITU KINAKWENDA SAWA KUHUSU SIMBA DAY - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 8 September 2021

SIMBA:KILA KITU KINAKWENDA SAWA KUHUSU SIMBA DAY

 


KUELEKEA katika tamasha la Simba Day, linalotarajiwa kufanyika Septemba 19, Uwanja wa Mkapa, uongozi wa timu hiyo umesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

Kwa sasa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu,Didier Gomes kipo Arusha,ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wanaendelea salama na mazoezi katika jiji la utalii Tanzania,  Arusha.

"Kuelekea katika Simba Day kila kitu kipo sawa hivyo ni suala la mashabiki kuweza kujitokeza kwa wingi kuona namna itakavyokuwa siku hiyo na tunaamini watafurahi.

"Tayari jezi ipo sokoni na inapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei hivyo kila shabiki kwa sasa ni muda wake kuipata jezi hiyo ambayo ina ubora wa hali ya juu,".

Septemba 13 inatarajiwa kuwa ni Wiki ya Simba ambapo watakuwa wakifanya matendo ya huruma kwa jamii pamoja na usafi.

Septemba 19 itakuwa ni siku ya tamasha rasmi ambapo mbali na kuwatambulisha wachezaji wao pia watatambulisha uzi na kutakuwa na mchezo kati ya Simba v TP Mazembe.

08Sep2021

No comments:

Post a Comment