Rais Kenyatta aanguka hesabu wakati wa hotuba wa kitaifa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 2 December 2021

Rais Kenyatta aanguka hesabu wakati wa hotuba wa kitaifa

 


Wakenya mtandaoni wamekuwa wakiangazia makosa ya hesabu yaliyofanywa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipokuwa akitoa hotuba ya kitaifa katika kikao cha pamoja cha mabunge ya nchi hiyo Jumanne.


Kiongozi huyo alitumia hotuba hiyo, ambayo huenda ikawa ya mwisho katika uongozi wake kwa kutegemea matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, kusifia mafanikio ya serikali yake.


Amekuwa uongozini kwa miaka minane tangu 2013.


Miongoni mwa aliyoyasifia ni mchango wa jeshi la nchi hiyo katika kufufua shirika la nyama nchini humo linalomilikiwa na serikali linalofahamika kama Kenya Meat Commission (KMC).


Lakini alikosea katika hesabu wakati akiangazia mafanikio katika kufufua shirika hilo.


Alisema chini ya uongozi wa jeshi, baada ya kipindi cha miezi michache tu, KMC sasa imekuwa ikikusanya jumla ya shilingi milioni moja za Kenya ($8,900; £6,700) katika moja ya vituo vyake ambavyo havipokei pesa taslimu.


Alisema awali kituo hicho kilikuwa kikikusanya Sh8,000 pekee. “Hii milioni moja ni sawa na shilingi za Kenya 30 milioni kila mwezi, na 3.6 bilioni kila mwaka katika kituo kimoja tu,” alisema.


Lakini hesabu hiyo haijakaa sawa. Ukizingatia kwamba kuna miezi 12 katika mwaka mmoja, takwimu sahihi ilifaa kuwa 360 milioni shilingi za Kenya na wala sio Sh3.6 bilioni.


Rais Kenyatta anaonekana pia kuanguka mtihani alipokuwa akizungumzia upanuzi wa uwezo wa Kenya wa kuzalisha umeme wakati wa utawala wake.


Alisema alipochukua uongozi mwaka 2013, uwezo wa Kenya ulikuwa wa kuzalisha megawati 1,300 na kwamba uwezo huo umeongezeka maradufu na kufikia megawati 2,600.


"Hii nis awa na megawati 325 zilizoongezwa kila mwaka chini ya utawala wangu,” alisema.


Tena, kuna makosa hapa kwani ongezeko la megawati 1,300 katika kipindi cha miaka minane nis awa na megawati 162 kila mwaka, na wala sio megawati 325 kama alivyosema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here