Kilo 1,989,418 za korosho ghafi zauzwa na RUNALI katika mnada wa kumi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Saturday, 8 January 2022

Kilo 1,989,418 za korosho ghafi zauzwa na RUNALI katika mnada wa kumi


Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi, leo kimefanikiwa kuuza kilo 1,989,418 za korosho ghafi  kupitia mnada wa kumi kwa msimu wa 2021/2022. 


Katika mnada huo uliofanyika leo mjini Nachingwea katika eneo la ofisi kuu ya chama hicho bei ya juu ilikuwa shilingi 1,780 na bei ya chini ni shilingi 1,670 kila kilo moja. Huku korosho za daraja la pili ambazo ni kilo 20,462 zimenunuliwa kwa shilingi 1,400 kila kilo moja. 


Kwamujibu wa meneja mkuu wa RUNALI, Jahida Hassan kwamba malipo ya wakulima waliouza korosho zao kupitia mnada wa tisa yamefanyika. Nakwamba wakulima hao wameshaingiziwa fedha zao kwenye akaunti zao. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here