Diamond Platinumz: Video ya wimbo mpya Gidi yakosolewa mitandaoni Marekani - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 22 February 2022

Diamond Platinumz: Video ya wimbo mpya Gidi yakosolewa mitandaoni Marekani

 

.

CHANZO CHA PICHA,DIAMOND PLATINUMZ

Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz anakosolewa mtandaoni kwa kuangazia bendera ya Shirikisho kwenye video ya wimbo wake mpya.

Shirikisho lilikuwa ni kundi la majimbo ya kusini ambayo yalipigana kudumisha utumwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani - na bendera hizo zinaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Moja ya matukio ya video ya Diamond katika wimbo wa Gidi ina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonkeano wa Cowboy.

Baadhi ya watumiaji wa Twitter wametoa hisia zao kuhusiana na video ya msanii huyo."Bendera ya Muungano katika video yako inasumbua,"aliandika mtumiaji mmoja.

"Bendera ya Muungano?"Clyde Blaise aliandika na kujuumisha emoji ya pipa la taka.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Kufikia sasa Diamond hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.

Diamond ambaye ndiye msanii maarufu zaidi katika eneo la Afrika mashariki hajaepuka migogoro katika siku za hivi karibuni.

Mwaka uliopita msanii huyo maarufu alijipata mashakani miongoni mwa wapenzi wa tuzo za BET.

Zaidi ya watu 20,000 walitia saini pingamizi mtandaoni wakitaka wasimamizi wa tuzo hizo kumpiga marufuku mwanamuziki huyo baada ya kuteuliwa kuwania orodha ya mwanamuziki bora wa kimataifa.

Nyota huyo wa muziki wa bongo Fleva alikuwa akituhumiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali Change Tanzania kwa kuunga mkono kile kilichodaiwa kuwa uongozi wa kiimla wa aliykuwa rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here