BIASHARA UNITED KATIKA BIASHARA YA KUSAKA POINTI TATU LEO - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 21 February 2022

BIASHARA UNITED KATIKA BIASHARA YA KUSAKA POINTI TATU LEO

 

BIASHARA United ya Mara leo inatarajiwa kushuka Uwanja wa CCM Kirumba kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC ya Dar.

Mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa Uwanja wa Karume ila miundombinu ya Karume haijawa rafiki.

Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu, Vivier Bahati imejikusanyia pointi 12 baada ya kucheza mechi 14.

Inakutana na Azam FC yenye pointi 24 ikiwa imecheza mechi 14 hivyo mechi ya leo kwa timu zote ni hesabu za kukamilisha mzunguko wa kwanza.

Ikumbukwe kwamba Bahati amewahi kuinoa Azam FC msimu huu kabla ya kuondoka pamoja na Kocha Mkuu, George Lwandamina hivyo anakutana na timu ambayo anatambua mbinu zake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here