Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo ameukataa mkataba wa kugawana mapato ya mafuta uliotiwa saini na wizara ya mafuta ya nchi hiyo na kampuni ya Marekani.
Kampuni ya uchimbaji wa mafuta ya Coastline Exploration imesema imesaini mikataba saba inayohusiana na utafutaji wa mafuta na gesi nje ya nchi.
"Somalia ina mabonde makubwa zaidi ambayo bado hayajachimbwa yaliyopo kwenye kitako cha maji joto duniani. Tunaheshima na furaha kuwa sehemu ya maendeleo yake ya baadaye," iliongeza katika taarifa hiyo.
Lakini taarifa kutoka kwa rais wa Somalia ilitangaza "kubatilishwa" kwa makubaliano hayo, ikisema Bwana Farmaajo hakushauriwa.
Taarifa hiyo Iliongeza kuwa makubaliano hayo yanakiuka amri ya rais inayokataza makubaliano kama hayo wakati wa mwaka wa uchaguzi.
Wizara ya mafuta na kampuni ya uchunguzi wa mafuta bado hazijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa hiyo ya rais.
Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble pia amekataa mkataba huo. Alidai kuwa wizara ya mafuta imetia saini "makubaliano yasiyo halali" ambayo yanaweka hatarini rasilimali za Somalia na kizazi kijacho".
Pia ameitaka wizara ya mambo ya ndani kuanzisha uchunguzi kuhusu suala hilo.
Hatua hiyo inaonyesha ukosefu wa uratibu miongoni mwa idara mbalimbali za serikali, wakati nchi ikijiandaa kukamilisha uchaguzi uliocheleweshwa kwa

No comments:
Post a Comment