Mwalimu wa shule ya Kiislamu aliyebaka wanafunzi 13 ahukumiwa kifungo cha maisha jela - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 16 February 2022

Mwalimu wa shule ya Kiislamu aliyebaka wanafunzi 13 ahukumiwa kifungo cha maisha jela

 

Wirawan alikuwa mmiliki na mwalimu wa shule ya bweni ya Indonesia
Image caption: Wirawan alikuwa mmiliki na mwalimu wa shule ya bweni ya Indonesia

Mahakama moja ya Indonesia siku ya Jumanne ilimuhukumu mwalimu wa somo la dini ya Kiislamu kifungo cha maisha jela kwa kuwabaka wanafunzi 13 wa kike.

Wanane kati yao walio na umri wa kati ya miaka 12 hadi 16 ni wajawazito kulingana na uchunguzi wa polisi.

Kesi hiyo inaangazia unyanyasaji katika baadhi ya shule za mabweni ambazo nyingi ni vituo vya mafunzo ya kiislamu.

Jaji aliamuru kwamba mwalimu Herry Wirawan, aliwanyanyasa kingono wanafunzi hao na kwamba baadhi yao walijeruhiwa vibaya.

Wirawan
Image caption: Watetezi wa kesi yake wamekuwa wakifanya kazi ili nakala halisi ya taarifa hii ipatikane mtandaoni.

Tabia ya Wirawan iligunduliwa mnamo mwezi Mei mwaka uliopita wakati mzazi wa msichana mmoja alipotangaza kwamba mwanawe wa kike ni mjamzito.

Viongozi wa mashtaka walimtaka mwalimu huyo kuhukumiwa kifo ama hata kuchinjwa kwasababu uhalifu alioutenda ulikuwa mbaya na ulifanyika kati ya mwaka 2016 hadi 2021.

Serikali ya Jakarta imetangaza kwamba itawalipa karibia dola 6000 kama fidia kila msichana aliyeathirika.

No comments:

Post a Comment