Tanzania kuanza kutengeneza chanjo ya corona - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 16 February 2022

Tanzania kuanza kutengeneza chanjo ya corona

 

Tanzania inalenga kuuza chanjo kwa majirani zake
Image caption: Tanzania inalenga kuuza chanjo kwa majirani zake

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali yake inataka kuanzisha kiwanda cha utengenezaji wa chanjo kama njia moja ya kutimiza mipango ya serikali ya kukabiliana na ugonjwa wa corona na magonjwa mengineo.

Akizungumza na Rais wa baraza la Ulaya, Bwana Charles Michel huko Brussels hapo jana, alisema kuwa Tanzania inataka kuwa muuzaji wa chanjo za kuokoa maisha kwa jamii ya Afrika Mashiriki (EAC) na nchi washirika wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais ambaye yuko kwenye ziara rasmi huko Ubelgiji, alisema kuna uwezekano Tanzania ikatumia hadi bilioni 216 za Tanzania hadi kufikia mwaka 2030 ili kuagiza chanjo kutoka nje ya nchi akisisitizia umuhimu wa kuwa na kiwanda cha uzalishaji ndani ya nchi.

‘’Tanzania ingependa kuwasilisha pendekezo hili na natazamia kwa hamu kuungwa mkono kwa wazo hili na kufanikiwa. Nina amini, mpango huu ukitekelezwa, utafungua fursa zingine na kuimarisha uhusiano wetu zaidi,’’ alisema.

Tangu kuanzishwa kwa ushirikiano na EU mwaka 1975, Tanzania imekuwa ikipata misaada ya maendeleo yenye thamani ya trilioni 5.98 pesa za Tanzania huku ikiwa imesalia kuwa moja ya mshirika muhimu kwa nchi hiyo

No comments:

Post a Comment