DC MOYO AWATAKA WANAWAKE IRINGA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI IRINGA. - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday 8 March 2022

DC MOYO AWATAKA WANAWAKE IRINGA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI IRINGA.

 


Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akihutubia wanawake waliokuwa wamejitokeza katika siku ya wanawake wilaya ya Iringa hasa halmashauri ya wilaya ya Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo   akipata maelezo kutoka kwa mjasiliamali mwanamke kutoka halmashauri ya Iringa siku ya wanawake wilaya ya Iringa hasa halmashauri ya wilaya ya Iringa 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo   akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mwanamke mjasiliamali siku ya wanawake wilaya ya Iringa hasa halmashauri ya wilaya ya Iringa 
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akigawa msaada wa taulo za kike kwa wanafunziwa kike waliokuwa wamehudhuri sherehe hizo
Baadhi ya wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Iringa wakifurahia jambo huku wakisakata rumba wakiongozwa na afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Zainabu

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewataka wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa wanauwezo wa kuongoza kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anavyoiongoza Tanzania.

Akizungumza katika sherehe za siku ya wanawake wilaya ya Iringa,Moyo alisema kuwa serikali imekuwa ikihamasisha na kutoa fursa za mbalimbali kwa wanawake ili waendelee kujiamini katika nyazifa ambazo wanakuwa nazo kwenye madaraka waliyonayo.

Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa hawajiamini kutokana na dhana potofu za kujiona kuwa hawafai kuwa viongozi kutokana na kutojiamini na kutojithamini hivyo wanatakiwa kuanza kujiamini na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Moyo alisema kuwa kila mmoja ni kiongozi kwa asili bila kujali elimu,umri,jinsia na rangi bali kila mmoja ameumbwa na kupewa mamlaka ya kutawala mazingira yanayomzunguka hivyo ni wajibu wa wanawake kujitathimini na kugombea uongozi kwenye changuzi zozote zile.

Alisema kuwa serikali inatambua kuwa wanawake viongozi katika nyazifa mbalimbali ambazo wamechanguliwa kuwa kufanya kazi kwa uhodari mkubwa kwa kuishawishi jambii kupokea maono waliyonayo na hatimaye kuleta mabadiliko kwa jamiii yote.

Moyo alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakipewa fursa mbalimbali za kielimu na kiuchumi ambapo wamekuwa wakifanya vizuri kuliko hata baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wakiaminiwa kwenye fursa hizo.

Aidha moyo alisema kuwa wanawake wamekuwa viongozi wenye unyenyekevu na uadilifu wameonyesha mafanikio,wakomavu na wanaongoza kwa malengo ambayo wanakusudia kuyalenga kuleta maendeleo kwa jamii husika.

Moyo alisema kuwa zaidi ya wanawake 16,000 wilaya ya Iringa wamepata hati milikiza kimila kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2021/2022 ambapo jumla ya kiasi cha shilingi 328,000,000 kimetolewa mkopo kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu lengo likiwa ni kukuza uchumi wao.

Moyo amewataja wanawake Kuwa Mfano Bora wa kuigwa katika masuala ya Uongozi kutokana na kuteketeza wajibu wao Kwa kutanguliza mbele Uzalendo, Uadilifu, uwajibikaji wenye maslahi mapana Kwa Taifa.

Moyo amesema Maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu nchini yamedhihirisha Nguvu ya wanawake katika Uwajibikaji na uchocheaji wa maendeleo Kwa Taifa huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassani Kwa Kuwa Kiongozi wa Mfano na mwenye maono mapana ya mendeleo.

Kiongozi huyo wa Wilaya Iringa ameyasema Hayo Wakati wa sherehe za Siku ya wanawake katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwasisitiza wanawake kuendelea kuwania fursa mbalimbali za uongozi Ili kulitumikia Taifa na kuchochea maendeleo.

Moyo alimalizia kwa kusema kuwahimiza wananchi kujitokeza kwenye zoezi la sensa ya watu na makama kama ambayo kauli mbiu ya siku ya wanawake inavyosisitiza “Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu:tujitokeze kuhesabiwa”.

Kwa mbunge wa jimbo la Kalenga Jakson Kiswaga alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi wa mfano kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassani amekuwa anaongoza taifa hili kwa weledi mkubwa.

Alisema kuwa wanawake mnatakiwa kijiamni na kuonyesha kuwa mnaweza kuwa viongozi imara kama amvyo Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassani Kwa Kuwa Kiongozi wa Mfano na mwenye maono mapana ya mendeleo.

Kiswaga alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassani kupitia serikali ya awamu ya sita anayoingoza amefanikiwa kutoa fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwenye jimbo la kalenga ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,vituo vya afya,miradi ya maji,miundombinu ya barabara na fedha kwa ajili ya mikopo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here