DED LUDEWA: WATAKAONG'OA VIBAO VYA ANUANI YA MAKAZI KUKIONA - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday 9 March 2022

DED LUDEWA: WATAKAONG'OA VIBAO VYA ANUANI YA MAKAZI KUKIONA

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias ametoa onyo kwa watu watakao onekana kung'oa vibao vya anuani ya makazi na kwenda kuuza kama vyuma chakavu hivyo kwa watakao bainikia watachukuliwa hatua za kisheria.


 Hayo ameyasema alipokuwa katika hafla ya siku ya wanawake wilayani humo na kuongeza kuwa kuna mikoa ambayo zoezi hili la vibao vya makazi tayari lilifanyika lakini watu waling'oa vibao na kuviuza hivyo katika Halmashauri yake hatarajii jambo hilo litokee ambapo amewataka viongozi wote wa ngazi ya kata na vijiji pamoja na wananchi kuvilinda vibao hivyo ili visiharibiwe.

"Viongozi wote wa kata na vijiji ninaomba mkahakikishe vibao hivi vinakaa katika hali ya usalama, nanyi wananchi mnatakiwa kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie ili kuhakikisha Halmashauri yetu inakaa katika mpangilio mzuri wa mitaa", Amesema Mkurugenzi.

Sanjari na hilo pia amewataka wakazi wote wa wilaya hiyo kujiandaa kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa Sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

 Amesema kufanikiwa kwa zoezi hilo kutaisadia serikali kupanga shughuli mbalimbali za maendeleo kulingana na idadi ya watu katika eneo husika hivyo wananchi wajitomeze kuhesabiwa.

Amesema kwa sasa serikali imeanza zoezi hilo kwa kuainisha makazi na kuzitambua barabara mbalimbali ambapo tayari baadhi ya barabara zimeshaanza kuwekewa vibao hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha jambo hilo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here