BBC imefichua jinsi utamaduni na kukataa kunaficha kiwango uhalisia wa unyanyasaji wa kijinsia unaotekelezwa na makasisi nchini Italia.
Kesi moja ya kushtua ambayo tumeizamia inafichua jinsi wanyanyasaji Kanisani wanaweza kuepuka haki.
Tahadhari: Taarifa hii ina maelezo ambayo yanaweza kukera wasomaji.
Tutamwita "Mario".Anarudi nyuma kidogo tunapopeana mikono, bado hayuko sawa na kusalimiana kwa kugusana mkono.
Na kwa swali langu la kwanza ; "Unaendeleaje? " ambayo nilitarajia ingemrahisishia taratibu kumfanya kwa huru katika mazungumzo yetu, na mara ghafla akaanza kulia.
"Mahojiano haya yananikumbusha yote yaliyopita," anagugumia, na kushindwa kutoa maneno hayo kupitia machozi yake.
Mario hajawahi kuzungumza kabla na mwandishi wa habari kuhusu kile anachokiita "utumwa wake wa ngono" mikononi mwa kasisi wake wa utoto.
Safari yetu itatupeleka kutoka kwa ushuhuda wa kutisha wa Mario, hadi kukabiliana na mnyanyasaji wake ana kwa ana - na hatimaye kutafuta majibu kutoka kwa wale ambao wamemruhusu kasisi kuendelea kuendesha Misa hadi leo.
Yake ni moja ya hadithi nyingi za unyanyasaji wa kijinsia wa makasisi nchini Italia, ambayo haijawahi kukabiliana na janga hilo.
Licha ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya makasisi wa nchi yoyote ile, na makao ya Kanisa Katoliki, Italia haihifadhi takwimu rasmi kuhusu suala hilo na hakujawahi kuwa na uchunguzi wa umma.
Katika kivuli cha Vatikani, dhambi za Italia zimefichwa chini ya pazia la giza.
"Bila shaka, niliambiwa kwamba ilikuwa siri," Mario anakumbuka, "kati yake, mimi na Yesu."
Siri hiyo ilikuwa, Mario anasema, miaka 16 ya unyanyasaji wa kutisha ambao alivumilia kutoka umri wa miaka minane, uliofanywa na kasisi aitwaye Padri Gianni Bekiaris.
Muhtasari wa kesi ya wakili wa Mario, ambao unajumuisha maelezo mengi ya kuvutia sana kuripotiwa, unaelezea ubakaji wa kwanza mwaka wa 1996 kama "uliopangwa".
Bekiaris alihifadhi chumba cha hoteli na kitanda kimoja kwa ajili yao wote wawili.
Baadaye, karatasi zilisoma, Mario aliachwa "katika maumivu na damu ... akilia kimya kimya".
Bekiaris baadaye aliwapa wazazi wa Mario "zawadi" ya bango linaloonyesha mahali hoteli ilikuwa - na mahali ambapo ubakaji unasemekana ulifanyika - ambapo aliandika tarehe na wakati wa wakati huo, pamoja na maneno: "Kwa kumbukumbu ya siku mbili tulizokaa kwenye baridi ya milimani."
Ilikuwa, ilionekana, ukumbusho uliopotoka wa uhalifu huo, na ishara ya jinsi kasisi huyo alivyomdanganya mtoto aliyeathiriwa kihisia, akifaidika na uhusiano mbaya wa Mario na baba yake.
Kesi hiyo inadai kuwa Bekiaris alimtishia Mario kunyamaza, "na kumwambia kilichotokea... pia lilikuwa kosa la mtoto".
Nilipokuwa ninakua, aliuliza wazazi wangu kama ningeweza kwenda kulala nyumbani kwake," Mario anakumbuka.
"Walikubali, ingawa niliomba wasingeweza."
Wazazi wake, bila kujua hali ya kutisha iliyokuwa ikitokea, walikuwa wakijionea fahari kupindukia kwamba mtu muhimu wa kanisani alithamini mtoto wao.
Jeraha hilo lilisababisha Mario kutumia dawa za kulevya, kuathirika kisaikolojia na kujaribu kujiua mara kwa mara.
"Aliiba roho nzuri niliyokuwa nayo," Mario anasema.
"Na jinamizi... ndoto zangu ni kuhusu vita na kutumia bunduki aina ya Kalashnikovs na mabomu ya kutupa kwa mkono."
Hatimaye, baada ya kufunguka kwa mtaalamu, Mario alianza kutafuta haki.
Hatua yake ya kwanza ilikuwa kumwendea mkuu wa Bekiaris, Askofu Ambrogio Spreafico.
Askofu Spreafico alianzisha kesi chini ya sheria ya kanuni - sheria ya Kanisa Katoliki, ambayo hutumika kushughulikia matatizo ya ndani.
Uamuzi ambao tumepata kutokana na kesi hiyo ya sheria ya kanuni unaonyesha majaji walimpata Bekiaris "dhahiri kuwa na hatia ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake" na kwamba, wakati akipinga baadhi ya maelezo ya unyanyasaji huo, "alikubali kutenda uhalifu".
Hata alifanya malipo ya €112,000 (£94,000) kwa Mario.
Lakini jopo hilo halikumtimua kasisi, kama Mario alivyoomba, badala yake liliamua kumpiga marufuku maisha yake yote "kusimamia kazi zake na watoto".
Wakiwa wamevunjika moyo, Mario na wakili wake waliwasilisha malalamiko ya uhalifu kwa polisi wa Italia.
Nyaraka ambazo tumeona katika kesi hii ya pili zinafichua kuwa majaji "hawakuwa na shaka juu ya ukweli wa madai hayo", na hivyo kuhakikisha kuwa "hakuna nafasi ya kuachiliwa kwa mshtakiwa".
Lakini chini ya mfumo mbovu wa kisheria wa Italia, kesi hiyo ilivuka mipaka ya sheria, ikimaanisha kuwa Bekiaris hangeweza kuhukumiwa.
Kesi hiyo inaonyesha utata wa vikwazo vya kisheria ambavyo vimenasa kesi za unyanyasaji wa kingono nchini Italia, na kuwanyima haki walionusurika - neno ambalo wanapendelea zaidi "wahasiriwa" - haki.
Sheria ya mipaka ya Italia - ambayo huanza wakati uhalifu unatendwa, badala ya kuripotiwa - inarekebishwa kwa sasa ili kukomesha kutumiwa kuzuia au kubatilisha mchakato wa kisheria, lakini mageuzi hayo hayatazamiwi tena.
Wakili wa Mario, Carla Corsetti, alituambia kikomo cha muda kimezuia visa vingi vya unyanyasaji wa ngono kutokana na miaka ambayo inaweza kuchukua kwa walionusurika kupona kutokana na uhalifu huo kiakili.
Lakini, anaongeza, tatizo hilo ni zaidi - kwa katiba ya Italia na Mkataba wa Lateran wa mwaka 1929 uliotiwa saini na dikteta aliyekuwa akitawala wakati huo Benito Mussolini, ambao uliipa Vatikani uhuru wa kisheria kutoka Italia.
Hili linawapa makasisi fursa ya kukimbilia sheria ya Vatikani kuliko ile ya Italia, ina wakinga dhidi ya haki ya Italia.
"Kupitia kuhifadhi Mkataba wa Lateran, sisi ni nchi yenye uhuru mdogo," Bi Corsetti anasema.
"Tunalipia ukweli huo kila siku na wanaolipa kwanza ni waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia."
Vatican chini ya Papa Francis imeongeza kasi polepole ya majaribio yake ya kukabiliana na kosa hilo, ikiharamisha, kwa mfano, matumizi ya kanuni ya ukimya inayoitwa "usiri wa kipapa".
Hivi karibuni, Baraza la Maaskofu wa Italia lilianzisha siku ya kwanza ya kitaifa ya sala ya Italia kwa ajili ya manusura wa unyanyasaji.
Lakini kwa wakosoaji, wanahisi hatua hizi zimechelewa sana kuanza kutekelezwa na mbaya zaidi hazitoshi.
Mnamo mwaka wa 2019, Umoja wa Mataifa uliitaka Italia kutekeleza uchunguzi huru na usio na upendeleo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia unaotekelezwa na makasisi.
Hata hivyo, wito wao umeanguka kwenye masikio ya viziwi na hadi sasa hakuna hatua iliyochukuliwa.
Mahali pengine ulimwenguni, maendeleo yanafanywa ili kuondosha usiri huo.
Ripoti moja huko Ufaransa mwaka jana ilipata kwamba tangu mwaka 1950, angalau watoto 216,000 walikuwa wametendwa vibaya huko na makasisi 3,200 hivi.
Italia ina makasisi zaidi ya mara mbili ya Ufaransa - lakini hakuna hesabu rasmi ya kesi za unyanyasaji.
Hata ndani ya kuta za Vatikani, wengine wameeleza kushangazwa na Italia kunyamazia suala hili.
Padri Hans Zollner, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulinzi katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Roma na mjumbe wa Tume ya Vatican ya kuwalinda watoto wadogo, ameitaka Italia kufuata mkondo wa Ufaransa na nchi nyingine zilizofanya uchunguzi wa uhalifu huu.
"Nchini Uingereza, Australia, Marekani, Ujerumani, jamii ilifikia hatua ya kukabiliana na suala hili na ndipo Kanisa pia lililazimika kukabiliana nalo - lakini ufahamu huu na uharaka wa kukabiliana nalo bado haujafika katika nchi hii," anasema.
Katika maeneo ambayo yamekabiliana na unyanyasaji wa makasisi, Padri Zollner anasema wastani wa 4-5% ya makasisi walishtakiwa au kuhukumiwa, akiongeza kuwa "kwa uwezekano wote, kungekuwa na idadi sawa inayotarajiwa nchini Italia".
Lakini kutokana na kukosekana kwa hesabu rasmi na bila ushirikiano wowote na taifa la Italia, imeachiwa kundi moja la kampeni nchini humo linaloshughulikia suala hilo kukusanya kile kinachoweza.
Francesco Zanardi - aliyenusurika mwenyewe - anaendesha chama kiitwacho The Abuse Network kutoka sehemu yake ndogo kaskazini mwa Italia.
"Tulipoanza kutafuta msaada na kuungwa mkono kisheria," anasema, "tuligonga ukuta".
Kwa kuchanganya taarifa za siri na ripoti za vyombo vya habari, amewaandika makasisi wa nchi hiyo ambao wameshukiwa, kuchunguzwa, au kuhukumiwa kwa unyanyasaji.
Na ameanzisha kundi la wanasheria tayari kushirikiana na manusura.
Bw. Zanardi amekokotoa hukumu 163 za makasisi nchini Italia katika kipindi cha miaka 15 iliyopita - lakini ana uhakika kwamba huo ni ukadiriaji wa chini.
"Italia ni kama sayari nyingine iliyo mbali na Ulaya," anasema.
"Kuna ukosefu wa wazi wa nia ya serikali kuingilia Kanisa, watoto wakiendelea kupata hasara.
Sehemu ya tatizo hapa ni utamaduni.
Italia mara nyingi ni ya kihafidhina zaidi katika masuala ya kijamii ikilinganishwa na nchi nyingine za Ulaya Magharibi.
Katika nchi ambayo zaidi ya 80% ya watu wanajitambulisha kuwa Wakatoliki, Kanisa, kwa Waitaliano wengi, ni muhimu kwa utambulisho wao kama familia - na mara nyingi linaweza kuonekana kuwa mamlaka isiyopingika.
Dhana hiyo ya ukimya na kutoguswa kwa Kanisa nchini Italia, kama Padri Zollner anavyoionyesha, imeruhusu baadhi ya makasisi wanaotuhumiwa kwa unyanyasaji kuwekwa katika mtandao wa vituo vya urekebishaji vinavyoendeshwa na Kanisa.
Vituo vingi kati ya hivi vipo kote nchini lakini kidogo kuvihusu vinajulikana.
Kuna mapadri wanaopelekwa katika vituo vya kurekebisha tabia.
Mapadri wanaotumwa kwenye vituo hivyo wana matatizo mbalimbali yakiwemo ya kucheza kamari na uraibu wa dawa za kulevya.
Lakini wengine pia wanatuhumiwa, chini ya uchunguzi au kesi kwa unyanyasaji wa ngono.
Marco Ermes Luparia, mwanzilishi, anakanusha vikali kwamba jumuiya yake ni "kimbilio la wakimbizi", akisisitiza kuwa badala yake ni mahali pa kutibiwa kwa makasisi ili kuzuia kudhulumiwa tena.
Wanyanyasaji hufuata kile anachokiita "mtu binafsi, mwendo mkali sana wa vikao viwili au vitatu vya matibabu ya kisaikolojia kwa wiki, ikifuatiwa na kizuizi cha jumla cha kutembea. Hawawezi hata kula chakula cha mchana nje."
Kwa walionusurika, miundo isiyoeleweka ambayo huwaepusha wanyanyasaji na kuwaficha, inaonyesha kwa mara nyingine tena mlolongo wa ushirikiano katika kuzika wahalifu.
"Maaskofu wanapaswa kushauri mamlaka zinazohusika kwamba padri anakuja kwetu," anasema, akipuuza madai ambayo jumuiya huwezesha Kanisa kuwalinda wanaonyanyasa.
"Leo askofu ambaye alifanya hivyo - itakuwa mwisho wake," anasema.
Hakuna utunzaji wa heshima kama huo kwa waathirika wengi wa unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na Mario, ambaye ufichaji wake unaendelea.
Mnyanyasaji wake, Gianni Bekiaris, anasalia kuwa kuhani hai bado katika dayosisi hiyo hiyo ambapo uhalifu unadaiwa kuanza - na bado chini ya uongozi wa Askofu Ambrogio Spreafico.
Tunatumia wiki kumfuatilia Bekiaris mtandaoni, kutafuta jinsi anavyosimama kusherehekea Misa katika makanisa mbalimbali katika zaidi ya mji mmoja, kabla ya kuonekana ameishiwa na hamasa tena.
Bado ameorodheshwa kama padri katika dayosisi ambapo unyanyasaji huo ulifanyika.
Tunapata hata picha zake akisherehekea Misa pamoja na watoto.
Hatimaye, katika eneo moja karibu na Roma, tunampata na kumkaribia.
Ninamuonyesha karatasi za majaribio tulizopata na picha za watoto waliohudhuria Misa yake. "Ninafanya kazi hapa," anajibu, akionyesha jengo analoishi, "na kwamba hakuna watoto."
Kisha ninatoa picha zake akiwa kanisani na watoto.
"Hao ni watu, si watoto wadogo," anasisitiza.
Anaanza kujificha ndani ya nyumba.
"Kwani, wewe ni wale watu wanaovutiwa kingono na watoto? Nauliza tu.
"Hivi ndivyo unavyosema," akajibu.
"Hapana, ndivyo mwathiriwa wako anasema," nikajiingiza kabla hajafunga mlango, na kusema "kwaheri" hivyo tu.
Ninamuuliza Padri Hans Zollner, kutoka Taasisi ya Ulinzi, nini kinadharia kifanyike kwa padri ambaye hatia yake ilitambuliwa katika kesi ya sheria ya kanuni, ambaye alikiri kutenda dhuluma na kulipa fidia.
Ananiambia kwamba, ingawa hajui kesi hiyo ninayozungumzia: "Ikiwa utaratibu utathibitisha kwamba alifanya uhalifu, anapaswa kufukuzwa kazi. Na ikiwa kuna aina yoyote ya shughuli inayomleta karibu na watoto, hiyo inaenda kinyume na hukumu.
Na bado, tunapozungumza na mkuu wa Bekiaris, Askofu Ambrogio Spreafico, kuhusu kwa nini hakuwa amemfukuza kasisi huyo licha ya ombi la moja kwa moja la Mario kufanya hivyo, akakana kutenda kosa lolote.
No comments:
Post a Comment