Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 20.03.2022: Pogba, Rudiger, Jesus, Azpilicueta, Neymar, Messi, Nunez - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday 20 March 2022

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 20.03.2022: Pogba, Rudiger, Jesus, Azpilicueta, Neymar, Messi, Nunez

 

Paul Pogba, Manchester United, Leeds United

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba (katikati)

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 29, amerejea katika darubini ya Barcelona baada ya klabu huyo ya Uhispania kusaini mkataba mnono wa udhamini. Mkataba wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa katika uwanja wa - Old Trafford unakamiliaka msimu huu wa joto. (Star)

Beki wa Ujerumani - Antonio Rudiger, ambaye mkataba wake katika klabu ya Chelsea unamalizika msimu huu wa joto, amekubali kujiunga na Juventus kwa mkataba wa miaka minnet. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)

Juventus watamnunua mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 24, ikiwa klabu hiyo ya Uingereza itafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21,kutoka Borussia Dortmund.(Star)

Gabriel Jesus

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Juventus kumnunua mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesu

Newcastle United wanataka kumsajili mshambulizi nyota wa Brazil Neymar,30, ambaye mkataba wake na Paris St-Germain unaendelea hadi 2025. (Fichajes, via Teamtalk)Mkufunzi wa Barcelona Xavi anasema mchezaji mwenzake wa zamani Lionel Messi, 34, "anakaribishwa muda wowote" uwanjani Nou Camp. Mshambuliaji huyo wa Argentina aliohamia PSG msimu uliopita. (Marca)

Messi hana nia ya kuondoka PSG na anapanga kukamilisha mkataba wake wa miaka miwili aliosaini na klabu hiyo ya Ufaransa. (Marca)

Messi

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Messi hana nia ya kuondoka PSG

Mlinzi wa Chelsea Cesar Azpilicueta amekubali kujiunga na Barcelona kwa mkataba wa bila malipo na uhamisho wa kiungo huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 32- unatarajiwa kukamilika msimu wa huu wa joto . (Football Insider)

Wakala wa kiungo wa kati wa Chelsea Jorginho anasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia wa miaka 30- anataka kurejea katika ligi ya Serie A. (Mirror)

Manchester United wanatathmini uwezekano wa kumnunua kipa wa Morocco na Sevilla Yassine Bounou, 30. (Mirror)

Manchester United wanamtaka mlinzi wa Uturuki wa miaka 24 Merih Demiral,ambaye yuko Atalantakwa mkopo kutoka Juventus.(Fanatik)

Atletico Madrid wanamtaka sana mshambuliaji wa Uruguay wa miak a22-Darwin Nunez, ambaye amesaidia Benfica kufuzu kwa robo fainali ya Champions League. (Fichajes -kwa Kihispania)

Atletico Madrid wamewasilisha dau la kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania Sergi Roberto, 30, ambaye anajiandaa kuondoka Barcelona mkataba wake utakapomalizika msimu huu wa joto. (Sport -kwa Kihispania)

Leeds United wana matumaini mlinzi wa Uingereza Luke Ayling,30, atakubali kusaini mkataba mpya, huku mkataba wake wa sasa unakamilika 2023. (Football Insider)

Newcastle United watamuachilia mlinzi wa IrelandKaskazini Jamal Lewis kuondoka msimu huu wa joto, klabu hiyo ya Tyneside club inataka karibu kumuuza kiungo huyo wa miaka 24 kwa £8m. (Football Insider)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here