Spika wa Bunge la Uganda Jacob Oulanyah amefariki dunia - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday 20 March 2022

Spika wa Bunge la Uganda Jacob Oulanyah amefariki dunia

 

Spika wa Bunge la Uganda

CHANZO CHA PICHA,SERIKALI YA UGANDA/TWITTER

Maelezo ya picha,

Spika wa Bunge la Uganda marehemu Jacob Oulanyah

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kifo cha spika wa Bunge la Uganda kwenye akaunti yake ya Twitter, leo Jumapili. Katika ujumbe wake, rais Mseveni alimtaja marehemu kama kada mzuri.

Kilichosababisha kifo cha Bw. Oulanyah hakijabainishwa, lakini alikuwa amelazwa hospitali nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Kusafirishwa kwake hadi Marekani kwa matibabu kulizua mjadala miongoni mwa Waganda, ambao walidai kuwa iligharimu pesa nyingi sana za walipa kodi.

Bw. Oulanyah alichukua hatamu ya uongozi wa bunge la Uganda mnamo Mei 2021. Alikuwa naibu spika kuanzia 2011.Alikuwa na sifa ya kuanzisha vikao vya bunge kwa wakati, na kila mara alitoa wito kwa wabunge kuimarisha ubora wa mijadala, kwa kujadili mambo waliyo na ufahamu wa kina.

Alikuwa mwanasheria na mwanasiasa wa muda mrefui. Aliwahi kuwa mbunge wa Eneo Bunge la Kaunti ya Omoro, kaskazini mwa nchi.

Bw. Oulanyah alikuwa miongoni mwa wanasiasa kutoka eneo hilo walioshiriki katika mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na waasi wa Lord's Resistance Army wali

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here